Skip to main content

UHUSIANO WA KUNDI LA DAMU NA UZITO

 


UHUSIANO WA KUNDI LA DAMU NA UZITO.

Kuna msemo unasema, ONE MAN'S FOOD IS ANOTHER ONE'S POISON. Ukiwa na maana ya kwamba, chakula kinachomnufaisha mtu mmoja, kwa mwingine ni hasara.

Dr. Peter J D'Adamo alifanya utafiti na kugundua ya kwamba kuna uhusiano mkubwa kati ya afya ya mtu pamoja na kundi la damu la mtu husika. Ndio akaja na msemo unaosema ya kwamba ONE MAN'S FOOD IS ANOTHER MAN'S POISON. Kwenye tafiti yake, aligundua ya kwamba afya ya mtu huimarika Zaidi endapo atakula kulingana na kundi lake la damu.

Hata kwenye swala la UZITO. Mtu wa kundi flani la damu anaweza kunenepa kwa kula vyakula vya aina flani, ambavyi vyakula hivyo hivyo akila mtu mwingine, basi atapungua.

Katika somo hili, tutaangalia uhusiano wa uzito wa mtu pamoja na kundi la damu.

BLOOD GROUP O

VYAKULA VINAVYOWAONGEZEA UZITO BLOOD GROUP O

·         Ngano na gluteni yake: kundi hili wakitumia ngano yenye gluten huingilia uzalishwaji wa insulin na hivyo kupelekea metabolism kua hafifu.

·         Mahindi ya sweetcorn: hufanya metabolism kua hafifu kwa sababu ya kuingiliwa uzalishaji wa insulin.

·         Maharagwe ya figo (kidney beans), maharage ya navy (madogo meupe), lenti: husababisha calories zisitumike kwa ufasaha.

·         Mboga jamii ya brassicas (inahusisha kabichi, broccoli, cauliflower): huzia hormone ya thyeroid kuzalishwa kwa kiwango kikubwa.

VYAKULA VINAVYOSAIDIA KUPUNGUZA UZITO KWA BLOOD GROUP O

·         Vyakula vya baharini (sea-food): huongeza uzalishwaji wa homoni ya thyroid.

·         Chumvi yenye iodine: huongeza uzalishwaji wa thyroid hormone.

·         Maini: yana vitamin B inayosaidia metabolism iwe vizuri.

·         Nyama nyekundu: huongeza metabolism kwa group O

·         Mboga ya kale, spinach: zinaongeza metabolism.

BLOOD GROUP A

VYAKULA VINAVYOWAONGEZEA UZITO

·         Nyama: haimeng'enywi vizuri na huhifadhiwa kama mafuta

·         Vyakula vya maziwa: vinachochea reaction ya insulin na kupelekea metabolism kua dhaifu

·         Maharagwe ya lima: yanafanya metabolism kua hafifu.

·         Ngano: ikitumika kwa kias kikubwa, inafanya misuli kua na acid na hivyo kufanya uhafifu wa utumiaji wa calories.

VYAKULA VINAVYOWAPUNGUZIA UZITO BLOOD GROUP A

·         Mafuta ya mbogamboga (vegetable oil): yanawezesha mmeng'enyo mzuri na kufanya maji yasibaki mengi mwilini. (fluid retention)

·         Vyakula vya soya: hufanya mmeng'enyo mzuri wa chakula, ufanisi wa metabolism na kuongeza kinga ya mwili.

·         Mbogamboga: ufanisi mzuri wa metabolism

·         Nanasi: unaongeza ufanisi wat umbo, na utumiaji mzuri wa calories.

BLOOD GROUP B

VYAKULA VINAVYOWAONGEZEA UZITO

·         Sweetcorn: inazuia uzalishwaji wa insulin na kupunguza ufanisi wa metabolism

·         Lenti: inasababisha sukari kushuka, inazuia virutubisho kufika mwilini vizuri na kupunguza metabolism.

·         Karanga: zinapunguza ufanisi wa metabolism, zinashusha sukari na kuzuia ufanisi wa kazi ya ini.

·         Mbegu za ufuta: kupungua kwa metabolism, na kushuka kwa sukari.

·         Ngano: kushusha sukari, kupungua kwa metabolism na kufanya chakula kitunzwe kama mafuta badala ya energy (nguvu)

VYAKULA VINAVYOPUNGUZA UZITO

·         Mboga za majani: huongeza metabolism

·         Nyama maini na mayai: huongeza metabolism

BLOOD GROUP AB

VYAKULA VINAVYOWAONGEZEA UZITO

·         Nyama nyekundu: mmeng'enyo wake ni wa tabu na huhifadhiwa kama mafuta.

·         Ngano: inashusha metabolism na utumiwaji wa calories.

·         Maharagwe ya figo, maharagwe ya lima, sweetcorn: huzuia uzalishwaji wa insulin na kushuka kwa sukari

·         Ngano: hushusha metabolism na utumiwaji wa calories mwilini.

VYAKULA VINAVYOWAPUNGUZIA UZITO

·         Tofu, vyakula vya baharini: zinaongeza metabolism

·         Mboga za majani: huongeza metabolism

·         Vyakula vya maziwa: vinaongeza ufanisi wa kuzalishwa kwa insulin

·         Matunda yenye alkaline (zabibu, nanasi, tikiti maji, apple n.k): yanaongeza alkaline kwenye misuli

·         Nanasi: linasaidia mmeng'enyo wa chakula na ufanisi wa kazi ya tumbo

Hii ni kutokana na utafiti wa Dr Peter D'Adamo.

Hapa nimejitahidi tu kuonyesha kipengele kinachohusiana na uzito. Ingawa yeye alielezea pamoja na afya kwa ujumla. Ambalo tutaangalia kwenye somo la siku nyingine.

Kwa msaada zaidi

whatsapp wa.me/255621068072 (bofya link)

mobile 0676068572/0753068572

 

Comments

Popular posts from this blog

DETOX YA SIKU 7. HATUA YA KWANZA KUPUNGUZA UNENE

  HATUA YA KWANZA KUPUNGUZA UNENE. Uzito Unaotakiwa kua nao Kulingana na Urefu Pamoja na Jinsia UREFU (CM) UREFU (FT & INCH) UZITO (KG)       MWANAUME MWANAMKE 147 4' 10" - 45-59 150 4' 11" - 45-60 152 5' 0" - 46-62 155 5' 1" 55-66 47-63 157 5' 2" 56-67 49-65 160 5' 3" 57-68 50-67 162 5' 4" 58-70 51-69 165 5' 5" 59-72 53-70 167 5' 6" 60-74 54-72 170 5' 7" 61-75 55-74 172 5' 8" 62-77 ...

FANYA HIVI KAMA UNASUMBULIWA NA CHUNUSI

  FANYA HIVI KAMA UNASUMBULIWA NA CHUNUSI. Chunusi ni vimbe zinazosababishwa na kuzibika kwa folikoli za nywele na mafuta ya ngozi (sebum), seli za ngozi zilizokufa, na protini zilizokufa. Kuziba huku kunavuta bakteria wa ngozi ambao husababisha uvimbe na kuongezeka kwa vimbe hizi. Sebum ni dutu yenye mafuta inayozalishwa na tezi za mafuta kwenye ngozi yako. Sebum inalinda ngozi, lakini unapozalishwa kupita kiasi, inaweza kuziba njia za ngozi, kufunga seli za ngozi zilizokufa, na kuvuta bakteria wa ngozi, hivyo kusababisha uvimbe na chunusi.   Uzalishaji wa sebum kupita kiasi unatokana na homoni za ngono zinazosambaa sana kwenye damu. Hii ndiyo sababu chunusi ni kawaida kwa vijana na watu wazima vijana. Protini inayojulikana kama Sex Hormone Binding Globulin (SHBG) inapunguza homoni za ngono zisizo na mpangilio.   SHBG inashikilia homoni hizi za ngono ili zisilete athari zisizohitajika kwenye seli na viungo kama ngozi. Homoni hizi za ngono ni estrogeni na testos...

BAWASIRI NA JINSI YA KUITIBU KWA NJIA ZA ASILI

 BAWASIRI NA JINSI YA KUITIBU KWA NJIA ZA ASILI.   💊💊💊💊💊💊💊💊💊💊💊💊💊   BAWASIRI NI NINI?   Bawasiri (kikundu, future, puru au mjiko ) ni hali ya kutuna kwa mishipa ya damu katika mfereji wa sehemu ya haja kubwa (anus). Kuna aina mbili za Bawasiri;   1. Bawasiri za ndani ( internal haemorroids )   2. Bawasiri za nje ( external haemorroids )  Bawasiri za ndani hua na dalili ya kupata kinyesi kilichokua na damu,  bawasiri za nje hua na dalili ya maumivu makali wakati wa kujisaidia pamoja na kinyama kutoka kwa nje.  NINI VISABABISHI VYA BAWASIRI?   1️⃣Historia ya familia, mara nyingi baadhi ya familia hukumbwa na changamoto hii. Na hua watu wa familia hiyo husika wanakua na hili tatizo. 2️⃣Kupata choo kigumu mara kwa mara husababisha mtu kutumia nguvu nyingi (straining) ambayo husababisha bawasiri kutokea. 3️⃣Unene (uzito uliopitiliza) hua ni kisababishi cha bawasiri kwa sababu ya kuongezeka kwa Rectal Vein Pressure. 4️⃣Ku...