kama umekua ukitumia diet ya aina flani kwa ajili ya kupungua uzito (na kueka afya nzuri kwa ujumla), basi utakua umeshajiuliza swali la namna hii.
Huu ndio ule msimu ambao kila kona unayopita wamepika chakula ambacho wewe ukitumia ni kinyume na Diet ambayo unaitumia katika kupungua uzito.
ONDOA SHAKA... FANYA YAFUATAYO:
Kabla ya yote, ni vyema ukafahamu ya kwamba ROME WAS NOT BUILT IN ONE DAY. Yaani Mji wa Roma haukujengwa ndani ya siku moja. bali ni mkusanyiko wa siku nyingi za ujenzi ndipo mji ukakamilika.
hivyo, hata kwa mtu ambae ana uzito mkubwa leo hii. sio kwamba aliongezeka ndani ya siku moja. Bali ni mkusanyiko wa siku nyingi ambazo hakua anakula vizuri au kua na mtindo mzuri wa maisha.
POINT YANGU NI IPI HASWA❓❔
kula kawaida siku ya siku kuu au msimu wa siku kuu hakutakufanya uharibu Diet yako ambayo umekua ukiendelea nayo. Hivyo bado unaweza kujumuika na ndugu jamaa na marafiki na mkala, kunywa na kufurahi pamoja.
ZINGATIA MAMBO YAFUATAYO🔰
1. Kula na ufurahie kinlichopikwa au utakachopika na kuandaa na wale uwapendao.
2. Baada ya msimu wa sikukuu kuisha, basi kesho yake rudi kwenye diet yako ya kuendelea na safari ya kua FIT pamoja na mwonekano mzuri.
3. Usisahau ya kwamba lengo lako ni lipi. hivyo ni vyema kurudi kwenye diet yako ya kupungua na kua na afya njema.
4. YOU ARE WHAT YOU EAT, vile unavyokula kila siku ndivyo hivyomutakavyokua.
5. Kumbuka ya kwamba, sio lazima uache Diet yako kwa msimu wa sikukuu, kama unaweza kuendelea hata kama ni sikukuu. Basi wewe ni Champion wa nguvu kwenye safari hii. kwani une nidhamu ya hali ya juu, na ni rahisi kushinda vita dhidi ya uzito mkubwa.
Kufikia hapo nikutakie maandalizi mema ya siku kuu ambazo zinakuja. nakutakia kheri, baraka pamoja na afya njema. (endapo utaitunza afya yako😉)
kwa msaada zaidi juu ya kupunguza uzito uliozidi,
whatsapp 0621068072 (wa.me/255621068072), mobile 0676068572/0753068572
By SAMUEL MACHA
FIT BY WAYNE
Asante kwa elimu mujarabu
ReplyDeleteShukran. Karibu sana
DeleteAsante sana doctor, maana nilishapata mawazo.
ReplyDeleteKaribu sana
DeleteRoma haikujengwa kwa siku moja bali ni mkusanyiko wa siku nyingi
ReplyDelete