Skip to main content

KWA NINI MZANI SIO NJIA BORA ZAIDI KUJUA KAMA UNAPUNGUA.


JE, MZANI AU KUJUA KILO NI SAHIHI KUJUA KAMA UNAPUNGUA?

Mara nyingi hutokea watu kukata tamaa wakati wapo kwenye safari yao ya kupungua kwa sababu ya kuangalia kilo zao kwenye mzani. Unakuta ameanza Diet mwezi uliopita, lakini akiangalia kilo zake kwenye mzani haoni mabadiliko makubwa...

Hapa nina solution mbili kama huyu mtu ni wewe
1. Usitumie mzani kwanza
2. Fahau jinsi ya kutumia mzani vizuri.

KWA NINI NIMESEMA USITUMIE MZANI KWANZA?

Kwa sababu mzani unakupa sehemu ndogo tu ya taarifa unazotakiwa kuzipata, yaani inakwambia uzito wako wa mwili kwa ujumla. 

Lakini mzani huo huo hautakupa taarifa kuhusu kiwango cha mafuta (FAT),  kiwango cha maji yaliopo mwilini, uzito wa mifupa, uzito wa misuli N.K

hivi vyote nilivyovitaja vinachangia uzito kwenye mwili wako. sasa lengo letu ni kupunguza mafuta, lakini sio kupunguza misuli au kitu kingine.

Ni vyema kufahamu ya kwamba, kilo utakazopima kwenye mzani hazikupi taarifa ya kwamba umepungua mafuta kwa kiasi gani. 

Angalia picha ya hawa watu wawili hapa chini

Ukiangalia hao watu wawili hapo juu, utagundua ya kwamba wote wana uzito unaofanana. lakini miili yao ni tofauti kabisa.

1. Mtu wa upande wa kushoto, ana kiwango kikubwa cha mafuta, na anaonekana mnene.
2. Mtu wa upande wa kulia, hana kiwango kikubwa cha mafuta, na anaonekana kua na mwili mzuri.

Japokua wote wana uzito unaofanana, mtu wa 2 anaonekana kua na afya na mwili mzuri zaidi ya mtu wa 1.

Japokua Mtu ni huyo huyo mmoja, ila amepoteza kiwango cha mafuta kwa kiasi kikubwa. lakini akipima uzito kwenye mzani, anaonekana kama vile ana kilo zile zile. ila kuna mabadiliko makubwa sana yametokea kwenye mwili wake.

JE, NINI CHA KUFANYA KUJUA KAMA UNAPUNGUA?

1. Jambo la kwanza, ni vyema ukawa unajipima tumbo lako au kiuno (waist or belly circumference) kwa kutumia tape measure. jipime mara moja kila wiki au kila baada ya wiki mbili. hii itakusaidia kujua maendeleo yako zaidi kuliko mzani.

2. Chunguza nguo zako. Unaweza ukagundua ya kwamba, kuna nguo ambazo mwanzoni zilikua zinabana lakini sasa zinakutosha vizuri. au ambazo zilikua zinakutosha vizuri lakini kwa sasa zinaowaya. ukiona hivi, maana yake unaelekea kuzuri katika safari yako ya kupungua.

3. Angalia mabadiliko unayopata katika mwili wako ambapo hapo awali kulikua hamna. kwa mfano:
  • unaweza ukakuta sasa hivi huchoki sana kama ambavyo mwanzoni ulikua unajiskia mchovu kila wakati
  • unaweza ukawa unajiskia na nguvu zaidi kuliko hapo awali.
  • unaweza ukajikuta hupendi tena yakula vyenye sukari au mafuta, na umezoea na kupenda vyakula vyenye afya zaidi.
  • maumivu ya miguu kupotea, au ukawa hukoromi tena kama mwanzo
  • unaweza kufanya vitu vingine vingi kwa urahisi wakati mwanzo ulikua huwezi, kama vile kutembea bila kuhema, kupanda ngazi, kuruka kamba n.k
Hivyo ni vyema ukaangalia mambo hayo yote, ndipo useme kama Diet yako inafanya kazi au la.

Nimalizie kwa msemo huu, YOU ARE WHAT YOU EAT, yaani wewe ni matokeo ya kile unachokula.

IF EATING HEALTHY IS EXPENSIVE, THEN WAIT UNTIL YOU SEE MEDICAL BILLS FOR NOT EATING HEALTHY EARLIER. mara nyingi watu wanasea ya kwamba kula vizuri ni gharama. ila subiri waje kuona gharama za kutibu magonjwa yatokanayo na kutokula vizuri hapo awali.

TUNZA SANA MWILI WAKO, NDIO SEHEMU PEKEE ULIYOPEWA KUISHI.

kwa msaada zaidi juu ya kupungua uzito na kua na afya bora

whatsapp 0621068072 au bonyeza link hii WHATSAPP

mobile 0753068572/0676068572

Imeandikwa na SAMUEL MACHA (CO)

FIT BY WAYNE
















Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

DETOX YA SIKU 7. HATUA YA KWANZA KUPUNGUZA UNENE

  HATUA YA KWANZA KUPUNGUZA UNENE. Uzito Unaotakiwa kua nao Kulingana na Urefu Pamoja na Jinsia UREFU (CM) UREFU (FT & INCH) UZITO (KG)       MWANAUME MWANAMKE 147 4' 10" - 45-59 150 4' 11" - 45-60 152 5' 0" - 46-62 155 5' 1" 55-66 47-63 157 5' 2" 56-67 49-65 160 5' 3" 57-68 50-67 162 5' 4" 58-70 51-69 165 5' 5" 59-72 53-70 167 5' 6" 60-74 54-72 170 5' 7" 61-75 55-74 172 5' 8" 62-77 ...

BAWASIRI NA JINSI YA KUITIBU KWA NJIA ZA ASILI

 BAWASIRI NA JINSI YA KUITIBU KWA NJIA ZA ASILI.   ๐Ÿ’Š๐Ÿ’Š๐Ÿ’Š๐Ÿ’Š๐Ÿ’Š๐Ÿ’Š๐Ÿ’Š๐Ÿ’Š๐Ÿ’Š๐Ÿ’Š๐Ÿ’Š๐Ÿ’Š๐Ÿ’Š   BAWASIRI NI NINI?   Bawasiri (kikundu, future, puru au mjiko ) ni hali ya kutuna kwa mishipa ya damu katika mfereji wa sehemu ya haja kubwa (anus). Kuna aina mbili za Bawasiri;   1. Bawasiri za ndani ( internal haemorroids )   2. Bawasiri za nje ( external haemorroids )  Bawasiri za ndani hua na dalili ya kupata kinyesi kilichokua na damu,  bawasiri za nje hua na dalili ya maumivu makali wakati wa kujisaidia pamoja na kinyama kutoka kwa nje.  NINI VISABABISHI VYA BAWASIRI?   1๏ธโƒฃHistoria ya familia, mara nyingi baadhi ya familia hukumbwa na changamoto hii. Na hua watu wa familia hiyo husika wanakua na hili tatizo. 2๏ธโƒฃKupata choo kigumu mara kwa mara husababisha mtu kutumia nguvu nyingi (straining) ambayo husababisha bawasiri kutokea. 3๏ธโƒฃUnene (uzito uliopitiliza) hua ni kisababishi cha bawasiri kwa sababu ya kuongezeka kwa Rectal Vein Pressure. 4๏ธโƒฃKu...

CALORIE ZA VYAKULA VYA TANZANIA

 CALORIES ZA VYAKULA TANZANIA   NINI MAANA YA CALORIE?    Calorie ni kiasi cha nishati kinachohitajika ili kuongeza joto la gramu moja ya maji (ยฐC). Kwa lugha nyepesi, calorie katika chakula hutoa nishati (energy) kwa njia ya joto ili miili yetu iweze kufanya kazi. Hii ni kwa sababu miili yetu huhifadhi na kuchoma calorie kama mafuta.  UHUSIANO WA CALORIE NA UZITO WA MWILI.  Kwa kawaida, kila chakula kina kiwango chake cha calorie. Hivyo unapokula chakula, unaingiza mwilini calorie kadhaa, na mwili wako pia unatumia calorie katika kuweka uhai. Lakini unapokula chakula, unaingiza calorie mwilini. Na mwili wako pia unatumia calorie kama nishati. Hivyo unapokula calorie nyingi kuliko mwili unavyoweza kutumia, zinahifadhiwa kama mafuta na utaongezeka uzito. Unapotumia calorie nyingi kuliko unavyoingiza mwilini, unapungua uzito. Na ukitumia kiasi sawa na unachoingiza, basi unabaki na uzito ule ule.   MWANADAMU ANAHITAJI WASTANI WA CALORIE NGAPI? ...