VYAKULA VINAVYOHITAJIKA
KATIKA AFYA YA NGOZI. (ANT-AGING FOODS)
Bila shaka unafaham ya kwamba kuna watu ambao wamekua na
makunyanzi na kuonekana wakubwa (wazee) kuliko umri wao halisi.
Lakini pia kuna ambao ngozi zao hulegea baada ya kupungua na
kuonekana kusinyaa pamoja na makunyanzi.
Collagen nip rotini muhimu sana katika kuipa ngoz afya, na
ndiyo inayohusika na kufanya ngozi iwe na hali ya kuvutika (elasticity)
Lishe inahusika sana kwa kiasi kikubwa kufanya ngozi yako iwe
vizuri na isiwe na makunyanzi au kuonekana yam zee kuliko umri wako.
VYAKULA MUHIMU KWA AFYA
YA NGOZI.
·
KITUNGUU SWAUMU: kina kiwango kikubwa cha sulfur
inayosaidia kuzalisha kiwango cha collagen. Hivyo jitahidi kutumia kitunguu
swaumu kama moja ya viungo vyako muhimu.
·
MAHARAGE: protini itokanayo na maharage
husaidia kuongeza kiwango cha collagen, bakuli moja la maharage lina wastani wa
gram 15 za protini ambazo zikifanyiwa mmeng'enyo wa chakula, amino acids
zinatumika kutengeneza collagen.
·
PILI-PILI HOHO: zina wingi wa Vitamin C ambayo husaidia
kuzalishwa kwa collagen, husaidia ngozi ipone haraka inapopata jeraha. Vile
vile hupambana inflammation hivyo kufanya ngozi isionekane kuzeeka haraka.
·
NYANYA: zina wingi wa Vitamin C pamoja na
Lycopene ambayo hutumia kufanya refreshment ya ngozi na kufanya usionekane mzee
au kua na ngozi yenye makunyanzi.
·
KUKU: nyama hii inawingi wa Niocene
pamoja na Vitamin B6 pamoja na kiwango kikubwa cha protini. Hizi zote husaidia
katika uzalishwaji wa collagen.
·
SAMAKI: sehemu kubwa ya samaki inayozalisha
collagen ni kichwa, macho pamoja na mifupa yake. Lakini pia ngozi ya samaki ina
kiwango kikubwa cha collagen. Ngozi yake ina kiwango kikubwa cha collagen
peptides.
·
MAYAI: sehemu nyeupe ya yai ina kiwango
kikubwa cha proline, ambayo ni amino acid inayosaidia uzalishwaji wa collagen.
Hivyo mtu anayeweza kutumia vyakula hivi atapata kiwango
kikubwa cha collagen. Na ukiwa na kiwango kikubwa cha collagen, inakufanya
uonekane mdogo Zaidi kwa sababu afya ya ngozi yako inakua nzuri sana.
EPUKA VYAKULA HIVI
UKITAKA NGOZI NZURI
·
SUKARI: inaongoza kwa kufanya ngozi
ionekane ya kizee au kuzeeka mapema kwa sababu inaingilia kazi ya collagen na
elastin. Sukari inapovunjwa mwilini, hujishikiza na collagen na kusababisha
makunyanzi. Lakini pia kiwango kikubwa cha sukari kwenye damu hufanya mtu
kuzeeka haraka na kuongezeka uzito.
·
ENERGY DRINKS: zimejaa sana kiwango kikubwa cha
acids, sukari na kemikali nyingine ambazo ni mbaya. Zina kiwango kikubwa cha
sodium na caffeine zinazosababisha ngozi kukosa maji (dehydration).
·
VYAKULA VINAVYOKAANGWA NA MAFUTA
MENGI: hivi hua na
kitu kinaitwa ADVANCED GKYCATION END PRODUCTS ambazo zinakufanya uzeeke haraka.
·
FAST FOODS (chipsi, pizza, burger): zina kiwango kikubwa cha Transfats
zinazosababisha mishipa ya dam kuziba na kusababisha mlundikano wa mafuta
kwenye mishipa ya damu.
·
POMBE: hushusha ufanisi wa ini ambalo ndio
kiungo kikubwa cha kuufanyia mwili wako Detox. (kuondoa taka mwili). Hii
husababisha kupata makunyanzi mapema.
·
VYAKULA VYENYE PILI PILI NYINGI: husababisha hali iitwayo ROSACEA kwenye
ngozi.
·
WANGA AU NGANO ILIYOKOBOLEWA: unapokula hizi, zisipotumika
mwilini hugeuzwa na kua sukari na husababisha kua na kiwango kikubwa cha sukari
kwenye damu. Na hii hupelekea kua na makunyanzi.
·
VYAKULA VYENYE CHUMVI NYINGI: husababisha kua na kiwango kikubwa
cha sodium na kusababisha kitu kinachoitwa WATER RETENTION (maji kubaki
mwilini). Na kusababisha ngozi iwe ya kizee kuliko umri wako. Ndio maana detox
diet nyingi hua hazina chumvi, au chumvi kidogo sana.
Lakini juu ya haya yote, jitahidi
sana kunywa maji mengi. Yanafaida kubwa sana kwenye afya ya ngozi na mwili kwa
ujumla.
Ngozi nzuri pia ina ambatana na
mazoezi. Sio lazima ufanye mazoezi makali, unaweza hata ukawa unatembea nusu
saa kwa siku. Hii itasaidia sana misuli iweze kua active na kuchangamsha
mwonekano wa ngozi yako.
Endelea kula vizuri, kumbuka ROMA
HAIKUJENGWA KWA SIKU MOJA. Hivyo usichoke kula vizuri. Kwani ndio unajenga
mwili wako uwe na afya bora.
Imeandikwa na SAMUEL MACHA.
FIT BY WAYNE.
👍
ReplyDeleteAsante sana my Dr matokeo binafsi nimeshayapata
ReplyDeleteThank u dr
ReplyDeleteAmina dr
ReplyDeleteAsante naaza kuifanyia Kazi...
ReplyDeleteNtaendelea kuvitumia, Asante kutukumbusha Dr
ReplyDeleteDaaah aiseee
ReplyDeleteBinafsi nakushukuru sana
ReplyDelete