Skip to main content

Posts

NAMNA YA KUFANYA MAZOEZI

  Mazoezi NAMNA YA KUFANYA MAZOEZI KWA AFYA. Mazoezi ni shughuli yoyote ya mwili ambayo huongeza au kudumisha utimamu wa mwili, afya na ustawi kwa ujumla. NI KWA NINI WATU HUFANYA MAZOEZI? kusaidia ukuaji wa mwili kuboresha nguvu ya mwili kupunguza kasi ya uzee kuboresha au kukuza misuli kuboresha mfumo wa moyo na mishipa kuboresha ujuzi wa riadha kupunguza uzito/unene au kudumisha uzito sahihi kuboresha afya starehe na sababu nyinginezo ISTILAHI MUHIMU ZA KUZIJUA Kabla ya kuona jinsi ya kufanya mazoezi kadhaa, ni vyema kufahamu istilahi chache muhimu ambazo zitakuongoza katika ufanyaji mazoezi yako. Istilahi nyingine utaendelea kujifunza kadiri ynavyoendelea kubobea katika mazoezi. REP : Hiki ni kifupisho cha neno Repeatition. katika mazoezi neno hili humaanisha kurudia kitendo flani. kwa mfano: mtu akisema 10 Reps, anamaanisha kufanya hicho kitendo husika mara 10. Kwa mtu ambae anapiga push up, akienda juu na chini amemaliza mara moja. hivyo 10 reps maana yake ni push ups 10. SET...

KWA NINI WATU WENYE UZITO MKUBWA HUHITAJI CHAKULA KINGI ZAIDI?

  WATU WENYE UZITO MKUBWA HUHITAJI CHAKULA KINGI ZAIDI. Bila shaka umeshawahi kusikia ama kuona neno CALORIE. Ikiwa na maana ya kiasi cha nishati kinachohitajika kuweza kuishi.  Hapo awali tulielezea ya kwamba, endapo mtu utaingiza calorie nyingi kuliko unazotumia, basi utaongezeka uzito. Na pia kama utatumia calorie nyingi zaidi ya unazoingiza mwili basi utapungua uzito. Kujua zaidi kuhusiana na Calorie kwenye vyakula tafadhali bonyeza  HAPA (CALORIE ZA VYAKULA) Tuangalie jambo moja, nalo ni BMR. Kirefu chake ni Basal Metabolic Rate.   Maana yake ni kiasi cha nishati kinachohitajika mwili kua hai wakati haufanyi shuhuli yoyote ile. BMR huchukua takribani 70% ya kiasi cha nishati kinachotumika kwa siku. Sasa kila mwili wa mwanadamu una BMR yake kulingana na Uzito wake ulivyo. Wenye uzito mkubwa hua na BMR kubwa zaidi kulinganisha na wenye uzito mdogo. Lakini pia wanaume hua na BMR kubwa zaidi kulinganisha na wanawake. Ili kuelewa zaidi kuhusiana na BMR, tazama ...

NJIA RAHISI JINSI YA KUANZA KUPUNGUZA UNENE/KITAMBI

  NJIA RAHISI JINSI YA KUANZA KUPUNGUZA UNENE/KITAMBI. Inakadiriwa ya kwamba, katika kila familia hapa Tanzania, hapakosekani walau mtu mmoja ambae ana uziro uliopitiliza. Yaani Obese. Wapo watu kadhaa ambao wamekua wakisema ya kwamba wao wana unene wa kurithi. Kwa sababu katika familia au ukoo wao wengi ni wanene. Lakini hili halina ukweli, Ila tu ni kwamba familia nyingi zinarithishana mtindo wa maisha. Na hivyo ndio maana unaweza kuona familia flani au ukoo flani wote ni wanene. Inapokuja swala la kupunguza unene, hamna njia za mkato kama ambavyo watu wengi hupendelea. Mtu anasahau ya kwamba hakunenepa ndani ya muda mfupi, bali alinenepa kwa muda mrefu. Lakini leo hii mtu atataka kupungua haraka sana ndani ya muda mfupi. ROMA HAIKUJENGWA KWA SIKU MOJA. Njia bora zaidi ya kupunguza Unene ni kwa kuzingatia ulaji sahihi pamoja na kubadilisha mtindo wa maisha kwa ujumla. Zipo dawa zinazosaidia kurahisisha safari ya kupunguza unene, lakini ieleweke ya kwamba, dawa hizi husaidia kura...

MADHARA YA KUTUMIA MKATE MWEUPE (NGANO ILIYOKOBOLEWA)

  Mkate Mweupe uliotengenezwa kwa ngano iliyokobolewa MADHARA YA KUTUMIA MKATE MWEUPE (NGANO ILIYOKOBOLEWA) Ngano ni moja wapo ya nafaka zinazotumika zaidi duniani. Ngano inashika namba 2, namba moja ikiwa ni mahindi na namba 3 ikiwa ni mchele kwa matumizi duniani.  Kuna mikate ya aina mbali mbali, na asilimia kubwa ya mikate hutengenezwa kwa kutumia Unga wa Ngano. kuna aina 2 za unga wa Ngano,  Unga wa Atta. (Unga wa Ngano ambao haujakobolewa) Unga wa Ngano uliokobolewa. (ngano nyeupe) Unga wa Ngano mweupe (uliokobolewa) ndio unaongoza kwa kutengeza mikate kwa asilimia kubwa. Ila madhara ya kutumia unga wa ngano uliokobolewa ni makubwa kuliko ambavyo watu wanafahamu. NINI MADHARA YA KUTUMIA NAFAKA ZILIZOKOBOLEWA? Kwa kawaida, mtu huchukua takribani dakika 5 kuweza kula kipande cha mkate wa unga wa Atta. (yaani mkate wa unga wa Ngano ambao haujakobolewa). Lakini mtu hutumia sekunde chache kuweza kula kipande cha mkate wa unga wa Ngano iliyokobolewa. (unga mweupe wa ngano)...

DETOX YA SIKU 7. HATUA YA KWANZA KUPUNGUZA UNENE

  HATUA YA KWANZA KUPUNGUZA UNENE. Uzito Unaotakiwa kua nao Kulingana na Urefu Pamoja na Jinsia UREFU (CM) UREFU (FT & INCH) UZITO (KG)       MWANAUME MWANAMKE 147 4' 10" - 45-59 150 4' 11" - 45-60 152 5' 0" - 46-62 155 5' 1" 55-66 47-63 157 5' 2" 56-67 49-65 160 5' 3" 57-68 50-67 162 5' 4" 58-70 51-69 165 5' 5" 59-72 53-70 167 5' 6" 60-74 54-72 170 5' 7" 61-75 55-74 172 5' 8" 62-77 ...