Mkate Mweupe uliotengenezwa kwa ngano iliyokobolewa |
MADHARA YA KUTUMIA MKATE MWEUPE (NGANO ILIYOKOBOLEWA)
Ngano ni moja wapo ya nafaka zinazotumika zaidi duniani. Ngano inashika namba 2, namba moja ikiwa ni mahindi na namba 3 ikiwa ni mchele kwa matumizi duniani.
Kuna mikate ya aina mbali mbali, na asilimia kubwa ya mikate hutengenezwa kwa kutumia Unga wa Ngano. kuna aina 2 za unga wa Ngano,
- Unga wa Atta. (Unga wa Ngano ambao haujakobolewa)
- Unga wa Ngano uliokobolewa. (ngano nyeupe)
NINI MADHARA YA KUTUMIA NAFAKA ZILIZOKOBOLEWA?
Kwa kawaida, mtu huchukua takribani dakika 5 kuweza kula kipande cha mkate wa unga wa Atta. (yaani mkate wa unga wa Ngano ambao haujakobolewa). Lakini mtu hutumia sekunde chache kuweza kula kipande cha mkate wa unga wa Ngano iliyokobolewa. (unga mweupe wa ngano).
Daktari anayefahamika kwa jina la Don Colbert aliwahi kusema "The whiter the bread, the sooner you are dead". Ikiwa na maana ya kwamba, kadiri unavyotumia Mkate mweupe (ngano iliyokobolewa), ndivyo unavyozidi kupunguza siku zako za kuishi.
Utumiaji wa nafaka zilizokobolewa ndio chanzo kikubwa cha Unene, kisukari, Magonjwa ya moyo, Saratani pamoja na magonjwa mengine mengi yasioambukiza.
KWA NINI MKATE MWEUPE (NGANO ILIYOKOBOLEWA NI MBAYA)
- Ngano iliyokobolewa hupoteza thamani yake ya lishe. (nutritional Value). Hii hupelekea kua na kiwango kikubwa cha sukari ambayo mwilini huhifadhiwa kama mafuta.
- Nyuzinyuzi (fiber) pamoja na Viini vyake huondolewa na kubakisha wanga (starch) peke yake
- Wanga (starch) hua oxidized, kuongezewa hydrogen (hydrogenation) pamoja na sukari ya ziada na hivyo kuifanya iwe na Glycemic Index ya juu sana. (Glycemic Index ni kiwango cha jinsi wanga unavyogeuzwa kua sukari mwilini na kuhifadhiwa kama mafuta badala ya kuchomwa kama nishati)
- Hufanyiwa Bleaching, kiasi kidogo cha chloride inaweza kugeuzwa na kua kemikali ambayo huongeza uwezekano wa kupata ugonjwa wa kisukari.
NINI CHA KUFANYA KUONDOKANA NA MADHARA HAYA?
Jambo kuu la kufanya ni kuachana na vyakula vitokanavyo na nafaka zilizokobolewa. Mfano Wali mweupe, tambi, sembe, Vyakula vya ngano iliyokobolewa kama vile chapati, maandazi, sambusa, kalmati, visheti, N.K
Badala yake ni vyema kutumia zaidi vyakula vya nafaka ambayo haijakobolewa kama vile dona, wali wa kahawia (wali wa brown), Unga wa Atta (ngano ambayo haijakobolewa) na nafaka nyinginezo ambazo hazijakobolewa.
Kujitahidi kutumia formula ya sahani ya mlo unaofaa. kama ambavyo inaelezewa katika makala hii. Bonyeza HAPA (Sahani ya Mlo Unaofaa)
Kufanya mazoezi walau mara 3 kwa wiki. Hakikisha unafanya mwili unakua active ili uweze kutumia na kuchoma mafuta kama nishati. Unaposhindwa kutumia wanga kama nishati, hugeuzwa na kuhifadhiwa kama mafuta mwilini. Na sio lazima kufanya mazoezi makali, ila unaweza kufanya mazoezi mepesi yanayoendana na mwili au uwezo wako, kushuka kituo kimoja kabla ya kituo husika ili ikupe nafasi ya kutembea, kutumia ngazi badala ya lift, kutembea kwa walau dakika 20 kwa siku N,K.
Kunywa maji ya kutosha kila siku kulingana na uzito wa mwili wako. kwa kawaida, katika kila kilo 20 za mwili wako, unatakiwa kunywa lita moja za maji. Mfano mtu mwenye kilo 80, kuna 20 mara 4 ndani yake. Hivyo atatakiwa kunywa walau lita 4 kwa siku ikiwa ni kiwango cha chini.
FAIDA ZA KUTUMIA NAFAKA AMBAZO HAZIJAKOBOLEWA.
- Zina wingi wa thamani ya lishe (nutritional value)
- Zina vipengele vyote muhimu kwa ajili ya kurutubisha mwili. (entire grain, kernel, bran na germ of endosperm). [zilizokobolewa hua na endosperm peke yake]
- Zina wingi wa nyuzinyuzi (dietary fiber)
- Zina wingi wa anti oxidants
- Zina wingi wa Protini inayoleta amino acid ya lysine
- Zina wingi wa madini kama vile magnesium, manganese, phosphorus pamoja na selenium
- Zina vitamini muhimu kama vile niacin, Vitamin B6 pamoja na Vitamin E.
UMUHIMU WA NYUZINYUZI (DIETARY FIBER)
- Husaidia kupunguza matatizo yatokanayo ya mmeng`enyo wa chakula kama vile kukosa choo na bawasiri.
- Husaidia kuondokana na matatizo ya magonjwa ya moyo.
- Husaidia kuondokana na matatizo ya kisukari.
- Husaidia kuweza kuondokana na changamoto ya unene uliopitiliza na kua na uzito sahihi.
Comments
Post a Comment