SAHANI YA MLO UNAOFAA
“Hati miliki © Chuo Kikuu cha Harvard. Kwa maelezo zaidi kuhusu Sahani ya Mlo Unaofaa, tafadhali tembelea Kitengo cha Lishe, Idaya ya Lishe, Chuo Kikuu cha Afya ya Jamii cha Harvard http://www.thenutritionsource.org na Majarida ya Afya ya Harvard, health.harvard.edu.” Sahani ya Mlo unaofaa, ambayo imebuniwa na wataalamu wa lishe kutoka Chuo Kikuu cha Afya ya Jamii, Harvard na kuhaririwa na wataalamu kutoka Harvard, ni muongozo wa mlo kamili unaofaa kwa afya-ikiwa utatumiwa kwenye sahani ya mlo ama kama chakula cha kufunga kwenye box. Bandika nakala kwenye fridge au kabati ili ikukumbushe kuandaa mlo kamili wenye afya!
Hakikisha unaweka aina mbalimbali zenye rangi tofauti. Viazi mbatata havihesabiwi kama mbogamboga katika Sahani ya Mlo unaofaaa kwa sababu ya madhara yake kwenye kiwango cha sukari mwilini.
Vyakula vinavyotokana na nafaka isiyokobolewa kama vile ulezi, mtama, mchele wa brown vinaathari kidogo katika kiwango cha sukari mwilini na utengenezaji wa insulini kuliko vyakula vinavyotokana na nafaka iliyokobolewa.
Samaki, Kuku, maharagwe, njugu, vyote ni vyakula vinavyoleta afya kutokana na protini-vinaweza kuchanganywa na kachumbari, na pia kwenye Sahani ya Mlo Unaofaa vinafaa kuchanganywa na mbogamboga. Punguza matumizi ya nyama nyekundu and epuka nyama za kusindikwa kama beconi na soseji.
Chagua mafuta yanayofaa ambayo yanatokana na mimea kama vile mizeituni, soya, mahindi, alizeti, karanga na mengineyo na epuka kutumia mafuta ambayo yameganda. Kumbuka kuwa alama ya “low-fat” kwenye makopo ya mafuta haimaanishi “mafuta yafaayo kwa afya”
Epuka vinywaji vyenye sukari, punguza matumizi ya maziwa na vyakula vitokanavyo na maziwa mpaka mara moja au mbili kwa siku, punguza matumizi ya juisi mpaka glass ndogo moja kwa siku.
Picha nyekundu ya mtu anayekimbia kwenye Sahani ya Mlo Unaofaa inakumbusha kuwa, kuweka mwili katika hali ya mazoezi ni muhimu pia katika kupunguza uzito. Ujumbe muhimu wa Sahani ya Mlo Unaofaa ni kusisitiza kuhusu Aina ya Mlo unaofaa
|
https://www.hsph.harvard.edu/nutritionsource/healthy-eating-plate/translations/swahili/
Sawa tumepata funzo
ReplyDelete