WATU WENYE UZITO MKUBWA HUHITAJI CHAKULA KINGI ZAIDI.
Bila shaka umeshawahi kusikia ama kuona neno CALORIE. Ikiwa na maana ya kiasi cha nishati kinachohitajika kuweza kuishi.
Hapo awali tulielezea ya kwamba, endapo mtu utaingiza calorie nyingi kuliko unazotumia, basi utaongezeka uzito. Na pia kama utatumia calorie nyingi zaidi ya unazoingiza mwili basi utapungua uzito.
Kujua zaidi kuhusiana na Calorie kwenye vyakula tafadhali bonyeza HAPA (CALORIE ZA VYAKULA)
Tuangalie jambo moja, nalo ni BMR. Kirefu chake ni Basal Metabolic Rate. Maana yake ni kiasi cha nishati kinachohitajika mwili kua hai wakati haufanyi shuhuli yoyote ile. BMR huchukua takribani 70% ya kiasi cha nishati kinachotumika kwa siku.
Sasa kila mwili wa mwanadamu una BMR yake kulingana na Uzito wake ulivyo. Wenye uzito mkubwa hua na BMR kubwa zaidi kulinganisha na wenye uzito mdogo. Lakini pia wanaume hua na BMR kubwa zaidi kulinganisha na wanawake.
Ili kuelewa zaidi kuhusiana na BMR, tazama mfano huu wa Bwanyenye...
Bwanyenye ni kijana mwenye uzito wa kilo 91. Kwa sasa BMR yake ni calorie 2500 akiwa ametulia bila kufanya chochote. Bwanyenye anachoshwa na uzito mkubwa, hivyo anafanya maamuzi ya kupunguza uzito kwa kubadilisha mtindo wake wa kula pamoja na kufanya maziezi.
Bwanyenye baada ya kufanikiwa kupunguza uzito, sasa ana kilo 73 na BMR yake ni calorie 2300 akiwa ametulia bila kufanya chochote.
Hivyo maana yake ni kwamba, Unapokua na uzito mkubwa zaidi, ndivyo jinsi unavyohitaji calorie nyingi ili uweze kuishi, na unapokua na uzito mdogo, unahitaji calorie chache zaidi.
Kadiri unavyopungua uzito au kuongezeka, na BMR yako hubadilika kutokana na kitu kinachoitwa Metabolic Adaptation. (hubadilika kulingana na uzito unaokua nao)
Ndio sababu kwa nini watu wanene au wenye uzito mkubwa mara nyingi hula sana kulinganisha na watu wenye uzito mdogo au wembamba.
Kwa msaada zaidi Juu ya kupunguza Unene
Comments
Post a Comment