Skip to main content

Posts

Showing posts from September, 2022

FAIDA 10 UTAKAZOZIPATA UKIACHANA NA MLO WA ASUBUHI.

 FAIDA 10 UTAKAZOZIPATA UKIACHANA NA MLO WA ASUBUHI. FAIDA 10 ZA KUTOKULA ASUBUHI. 1. UTIMAMU WA AKILI/ KUMBUKUMBU NZURI Unapokula chakula cha asubuhi, unafanya domapine zako zimwagike bila sababu za msingi na hivyo kufanya uzito katika ufanyaji kazi wa ubongo wako. Watu ambao hula mlo wa asubuhi hua wanapata uvivu na ufanisi wa kazi zao kwa siku husika hua mdogo kwa sababu ubongo unakua bize kutengeneza dopamine ambayo imemwagika (dysregulated dopamine) pamoja na kusimamia umeng`enywaji wa chakula. 2. ARI YENYE NGUVU (ENERGETIC SOUL) Kila alfajiri kuanzia mida ya saa 10, mwili wako huachilia homoni zijulikanazo kama counter-regulatory hormones ambazo hukusaidia kukupa nguvu ya kuweza kupambana na siku husika. Hata kama una kazi ngumu kwa asubuhi hiyo, mwili wako unaweza kukupatia nguvu inayojitosheleza wewe kufanya shuhuli zako pasipo shida yoyote. Watu ambao hula asubuhi hupata kitu kijulikanacho kama sugar crash ambapo miili yao hua dhaifu kwa sababu inakua bize kuweka

JE, MLO WA ASUBUHI (BREAKFAST) UNA FAIDA YOYOTE?

  JE, MLO WA ASUBUHI UNA FAIDA YOYOTE? MLO WA ASUBUHI HAUNA FAIDA YOYOTE KWAKO. Bila shaka umeshawahi kusikia au kuambiwa ya kwamba mlo wa asubuhi ni mlo wa muhimu kuliko mlo wowote ule. Tena ukaambiwa maneno kama vile ‘Kula mlo wa asubuhi kama mfalme, mlo wa mchana kama mtoto wa mfalme na mlo wa jioni kama ombaomba/maskini’ Je, kuna ukweli wowote kuhusiana na hili? Jibu ni HAPANA. Mlo wa asubuhi ni mlo usio na maana au faida yoyote kwako kuliko mlo wowote ule. NI KWA NINI MLO WA ASUBUHI HAUNA MAANA AU FAIDA YOYOTE KWAKO? Inapofika saa kumi alfajiri, mwili wako huachilia kiwango cha juu cha homoni aina nne.         I.             Glucagon       II.             Adrenaline     III.             Cortisol     IV.             Growth hormone Homoni hizi hupandisha kiwango chako cha sukari kwenye damu wakati wa alfajiri kupitia mfumo wa kibaiolojia ujulikanao kama DAWN PHENOMENON . (ndio mfumo ambao hufanya mwanaume au mtoto wa kiume awe amesimamisha uume wake wakati anapoamk

MADHARA YA PAMPERS (DIAPERS) KWA MTOTO

  MADHARA YA PAMPERS (DIAPERS) KWA WATOTO. Kwa wale ambao ni wakongwe kidogo, yaani waliozaliwa miaka ya 90 kurudi nyuma, wengi hawakuvalishwa pampers na wazazi wao, bali walivalishwa nepi au vinginevyo. Lakini miaka ya hivi karibuni na tunapoelekea, kila mtoto anavalishwa pampers kulingana na utandawazi unavyozidi. Kadiri siku zinavyozidi kwenda, ndivyo ambavyo mwanadamu anazidi kua mbali na asili yake na kuingia kwenye usasa ambao hauna chochote cha asili. Kadiri mwanadamu anavyoacha asili yake, ndivyo ambavyo matatizo ya ki afya huzidi Zaidi na Zaidi. Pampers za watoto zimetengenezwa na kemikali hatarishi ambazo huathiri afya ya mtoto ambae anakua. Kemikali hizo hufanya mambo yafuatayo; - ·          Huharibu ngozi ya mtoto na kusababisha mzio wa ngozi maeneo ya sehemu zake za siri. ·          Kemikali hizi hufyonzwa katika tishu za mwili na kusababisha shida katika kinga ya mwili wa mtoto anaeivaa pampers hiyo. ·          Kemikali hizi ni neurotoxic (husababisha shida

MADHARA YA SODA KATIKA MWILI WAKO

  MADHARA YA SODA KATIKA MWILI WAKO. Moja ni moja kati ya vinywaji vinavyopendwa na kutumiwa sana na watu wengi. Na mbaya Zaidi, hata watoto ambao hawana hatia hupewa soda na wazazi wao kwa madai ya kuwaonyesha upendo kwa kuwaburudisha. Lakini kitu ambacho hatukifahamu ni kwamba tunajichimbia makaburi wenyewe na kujiwekea nafasi ya kuumwa magonjwa ambayo yanatesa sana baadae na kuyatibu ni gharama kubwa sana. Soda imetengenezwa na vitu vingi vyenye sumu ambavyo havina faida yoyote katika mwili wa mwanadamu, lakini mbaya Zaidi ni kwamba vina madhara makubwa ambayo hua hayatokei kwa haraka bali huja taratibu katika maisha ya mwanadamu. KEMIKALI ZILIZOPO KATIKA CHUPA YA SODA NI; - ·          Carbonated water ·          High fructose corn syrup ·          Caramel ·          Phosphoric acid ·          Artificial flavouring ·          Caffeine. Hivyo wakati wowote ule unapokunywa chupa ya coca cola, fikiria unaingiza vitu vyote hivyo katika mwili wako ndani ya dakika ch

UZURI WA VIAZI VITAMU

  UZURI WA VIAZI VITAMU. Viazi vitamu ni moja kati ya vyakula vya wanga bora kabisa unavyoweza kula. Hii ni kwa sababu ni Wanga Tata, (Ccomplex carbohydrates), ikiwa inamaanisha havisababishi kupanda kwa insulin na hivyo hamna kupanda kwa sukari. Glucose iliyopo ndani yake huachiliwa taratibu kwa sababu vina wingi wa nyuzinyuzi. Kama unauwezo wa kuvipanda mwenyewe na kuvuna, ni bora Zaidi. Inapendekezwa, kama unavila basi ule na maganda yake kwa ajili ya kupata faiza zake zote (kama unaweza). Viazi vitamu husaidia kuleta uwiano wa bacteria wazuri wa kwenye utumbo ambao husababisha uzalishwaji wa Butyrate. Kazi ya Butyrate ni kulinda kuta za tumbo zisitoboke na kuvuja. Kumbuka ya kwamba, glucose sio adui endapo wewe ni mwembamba na hua unashuhulisha mwili. Bali fructose (inayopatikana kwenye sukari) ndio adui yetu mkubwa. Napendekeza utumie vya kuchemshwa, weka chumvi na ufurahie mlo wako. Pia unaweza kuvianika juani, na ukatengeneza unga wake ambao ni mzuri sana. Achana