Ulaji na mtindo mbaya wa maisha husababisha unene. |
MAZOEA/TABIA 10 ZA KUJENGA UDHIBITI WA KUONDOKANA NA UNENE.
Unene kupita kiasi ni tatizo la kiafya ulimwenguni kote. Uzito uliopitiliza ni kuwa na 10% hadi 19% zaidi ya uzito sahihi unaotakiwa kiafya.
Wakati Unene kupita kiasi ni kuwa na zaidi ya 20% ya uzito sahihi unaotakiwa kadiri ya urefu, jinsia na ukubwa wa mifupa.
Kiini cha tatizo hili ni kiasi kikubwa cha Kalori. Uzito huongezeka pale ambapo unakula kalori nyingi zaidi kuliko mwili wako uwezavyo kutumia. Kalori za ziada huhifadhiwa kama mafuta mwilini. Kwa kila kalori 3,500 za ziada inayopokelewa mwilini, nusu kilo ya uzito huongezeka.
UZITO SAHIHI UNAOTAKIWA KUA NAO KULINGANA NA UREFU PAMOJA NA JINSIA.
jedwali la uzito sahihi kulingana na urefu pamoja na jinsia. |
MAZOEA 10 YA KUJENGA UDHIBITI WA KUDUMU WA UZITO SAHIHI.
- Tumia vyakula vya mimea/nafaka ambazo hazijakobolewa, vyakula hivi hua na wingi wa nyuzinyuzi na viinilishe. (Ili kujua madhara ya nafaka zilizokobolewa, soma HAPA (madhara ya nafaka zilizokobolewa)
- Usiache kula kifungua kinywa kwa kutumia chakula chenye mchanganyiko wa nafaka mbali mbali pamoja na matunda.
- Tumia milo miwili au mitatu kwa siku katika nyakati maalum bila kula kitu chochote katikati ya milo.
- Kula chakula chako au tafuna taratibu, tumia muda kufurahia chakula chako, hii itasaidia chakula chako kusagwa vizuri tumboni.
- Kula matunda katika kukamilisha mlo wako badala ya kutumia vitu vya sukari kama vile soda au juisi.
- Usile chakula chako cha jioni/usiku kwa kuchelewa. (weka tabia ya kutokula zaidi ya saa 2 au 3 usiku, na usitumie vyakula vya wanga wakati wa usiku)
- Kunywa maji mengi badala ya kunywa juisi au soda.
- Fanya mazoezi kila siku walau kwa dakika 30 au tembea Hatua 10,000 kwa siku.
- Epuka vitu vyenye madhara kama vile pombe, tumbaku (sigara), kafeni, dawa za kulevya n.k)
- Fanya kitu chenye manufaa kama vile kusoma vitabu, kucheza na watoto, kutembea nk badala ya kukaa na kuangalia TV au kukaa tu na kula.
Kama ukiweza kuwa na tabia 10 zilizotajwa hapo juu na ukiweza kuzifanya sehemu ya maisha yako, basi tatizo la uzito uliopitiliza/unene litaondoka kwenye maisha yako.
Watu wengi hua wanatamani kuondokana na unene, lakini unapowaambia mambo ya kufanya ili waondokane na unene, hawafanyi. Hua wanataka kupungua kwa miujiza, sasa hamna miujiza katika kupunguza unene, ni lazima kufwata kanuni za kua na afya bora.
Hua napenda kusema ya kwamba, ROMA HAIKUJENGWA KWA SIKU MOJA. Hukua mnene ndani ya siku moja, bali ni siku nyingi, Hivyo usitafute njia za mkato, hazitakusaidia kwa muda mrefu.
Nakubali doctor Wyne.
ReplyDeletenashukuru sana
Delete