JINSI MWANAMKE
ANAVYOWEZA KUZUIA AU KUKABILIANA NA VIMBE KWENYE KIZAZI (FIBROIDS).
Fibroids ama vimbe kwenye kizazi ni tatizo la kihomoni ambalo
linatokea kwa mwanamke ambae yupo katika umri wake anaoweza kuzaa.
Hii humaanisha ya kwamba fibroids hua zinalishwa na homoni ya
oestrogen. Fibroids ni kama magugu ambayo huota shambani katika shamba ambalo
halifanyiwi palizi au limeachwa.
Wanawake walio katika hatari ya kupata fibroids ni;-
·
Wanawake
wenye umri kuanzia miaka 28, japokua hata chini ya miaka 28 wanaweza kupata.
·
Wanawake
wanene.
·
Wanawake
weusi (waafrika); hii ni kwa sababu ya ulaji pamoja na mtindo wa maisha.
·
Wanawake
wenye shida ya presha pamoja na kisukari.
·
Historia
ya familia kua na fibroids. Familia huambukizana epigenetics na endocrine disruptors
kutokana na tabia ya ulaji na mtindo wa maisha ya familia husika.
·
Wanawake
ambao hawajazaa. Haswa ambao wamefika miaka 30.
·
Wanawake
wenye upungudu wa Vitamin D.
·
Wanawake
wenye ulaji mbovu mfano matumizi ya sukari, nafaka zilizokobolewa, mafuta ya mbegu
pamoja na vyakula vilivyochakatwa.
·
Matumizi
ya soya, maziwa yaliyochakatwa
·
Pombe
kwa sababu ni oestrogenic.
DALILI ZA MWANAMKE
MWENYE FIBROIDS.
·
Kutokwa
na damu nyingi sana wakati wa hedhi.
·
Kutokwa
na damu katikati ya hedhi na hedhi nyingine (yaani siku ambazo sio za hedhi)
·
Maumivu
makali wakati wa hedhi.
·
Kupata
kitambi cha chini ambacho ni kigumu kupungua.
·
Kushindwa
kubeba ujauzio kwa sababu fibroids zinazuia kutungwa kwa mimba.
·
Mimba
kutoka mara kwa mara.
NJIA RAHISI ZA KUPONA
VIMBE KWENYE KIZAZI (FIBROIDS)
·
Kuacha
matumizi ya sukari pamoja na nafaka zilizokobolewa
·
Kuacha
matumizi ya mafuta ya mbegu
·
Kufunga
kula mara kwa mara/ kila siku
·
Kuacha
matumizi ya ngano
·
Kutembea
juani wakati wa asubuhi
·
Kuacha
matumizi ya pombe na sigara
·
Kupunguza
uzito kama ni mnene
·
Kupumzika
na kulala walau saa 8 kwa siku.
·
Kufanya
mazoezi walau mara 3 kwa wiki
Kitu kikubwa kinachotishia afya ya uzazi ni vitu
vinavyochochea na kusababisha uharibufu au mvurugiko wa homoni za mwanadamu.
Kabla ya mwanamke yoyote yule kukubali kufanyiwa upasuaji kwa
ajili ya vimbe kwenye kizazi (fibroids) ni vyema kwanza akabadilisha ulaji wake
pamoja na mtindo wa maisha.
Endapo utafanya upasuaji na huku vile visababishi vikuu bado
havijaondolewa, maana yake zitaturi tena katika maisha yako.
Reference: www.amerix.co.ke
Comments
Post a Comment