Skip to main content

Posts

Showing posts from October, 2022

P TATU ZA KUA NA AFYA NZURI

  P TATU ZA KUZINGATIA ILI UWE NA AFYA NZURI. Tupo katiika dunia ambayo watu wengi hupenda sana njia za mkato katika kila kitu. Na katika afya, wengi hukimbilia vidonge na dawa badala ya kubadilisha mtindo wa maisha yao ili waweze kuishi pasipo kutumia dawa ambazo mwisho wa siku zina madhara katika mwili.  Moja ya adui wakubwa ni UNENE, ni kwa sababu unene unakuanika katika kupata athari nyingi za ki afya mfano saratani, kisukari pamoja na magonjwa mengine mengi. Ila wengi hawataki kufanya hivyo wakidhani kuna vidonge vya kila tatizo wanalopata.  Dawa haziwezi kamwe kukuponya ugonjwa sugu, zitaondoa tu dalili kwa wakati huo na kukufanya uitegemee dawa hiyo katika maisha yako yote bila kupona kabisa. Utakua tu ukipata nafuu ili na kesho utumie tena na tena.  Chukulia mfano wa watu wenye vidonda vya tumbo, presha na kisukari. Kila siku watameza vidonge vitakavyowapa nafuu kwa muda mfupi, ila baadae wanarudi palepale. Maana yake ni kwamba kila siku itawabidi kutumia dawa hizo. Au

TATIZO LA KUTAPIKA/KICHEFUCHEFU UNAPOSAFIRI

  TATIZO LA KUTAPIKA AU KUHISI KICHEFUCHEFU UNAPOSAFIRI. Watu wengi sana wana hili tatizo. Tatizo hili hujulikana kama MOTION SICKNESS . Na lina sababu kuu 2         I.             ADRENAL GLAND FATIGUE       II.             GALL BLADDER/BILE DYSFUNCTION. 1. ADRENAL GLAND FATIGUE Adrenal glands hupatikana juu ya figo zako na huachilia homoni muhimu ijulikanayo kama CORTISOL. Cortisol husaidia tishu zako za mwili kuweza kukabiliana na hali za stress n.k ambazo ni; - ·          Inflammation ·          Motion (unapokua katika mwendo) ·          Height awareness (unapokua katika urefu mkubwa sana) ·          Kukagua kinga ya mwili ili isiweze kukushambulia (autoimmunity) Kama una cortisol ya kiwango cha chini sana, hupelekea shida ya chronic inflammation, kizunguzungu pamoja na kichefuchefu. Matokeo yake ni; -         I.             Kupata pumu au uzio (allergy)       II.             Kupoteza kumbukumbu     III.             Magonjwa ya Autoimmunity mfano lup

MAUMIVU YA KICHWA MARA KWA MARA

  MAUMIVU YA KICHWA MARA KWA MARA. Yawezekana hua unasumbuliwa au umeshaona mtu ambae hua anasumbuliwa na maumivu ya kichwa ya mara kwa mara. Na mara nyingi maumivu haya hua hayaishi hata kama ukimeza paracetamol au dawa yoyote ya kutuliza maumivu. Wengine huenda hospitali, kila vipimo wanavyofanyiwa huonyesha ya kwamba hawana shida yoyote ile. Mpaka wengine hudhania ya kwamba kuna mtu anawaloga. NI KWA NINI MAUMIVU HAYA HUTOKEA? Kisababishi kikuu hua ni upungufu wa madini ya Sodium mwilini. Kua na upungufu wa sodium kitaalam huitwa HYPONATRAEMIA. Watu wenye upungufu wa Sodium hua na shida kwenye pampu ya umeme katika seli zao ijulikanayo kama Sodium-Potassium Channel Pump. Pampu hii hutoa chaj za umeme kwa ajili ya kupeleka nguvu katika misuli na mfumo wa fahamu ili iweze kufanya kazi vizuri. Kukiwa na shida katika pampu hiyo, hutoa potassium kwa wingi sana katika seli za ubongo na hivyo kusababisha hali ya excitation katika chaneli za fahamu na matokeo yake kupata mau

UZITO HUPOTEA KIUNONI NA SIO KWENYE MZANI

  UZITO/UNENE HUPOTEA KIUNONI NA SIO KWENYE MZANI. Ukitaka kutambua mwenendo wako wa kupungua uzito au unene, basi tumia kiuno chako na wala usitumie mzani. Mzani hauwezi kukupa ufanisi wa kujua uzito au unene ambao umepungua. Mzani hua unakupa tu uhakika, lakini kiuhalisia haikuonyeshi maendeleo yako kwa ufasaha. Usitumie muda mwingi sana kuangalia mzani wako unasemaje, kwa sababu mizani tofauti hua na calibration ya tofauti na pia unapopima kwa nyakati tofauti hua unapata namba tofauti. NJIA BORA YA KUJUA UZITO AU UNENE ULIOPUNGUA NI IPI? Njia bora Zaidi ni WAIST-TO-HEIGHT RATIO (WSR). Lakini pia, kuna mambo kadhaa ambayo unaweza kuangalia na kujua ya kwamba unapata matokeo mazuri. Mfano wa njia hizo ni; - ·          Kupata usingizi mzuri ambao mwanzoni hukua unaupata. ·          Kutokupata njaa mara kwa mara na kushiba mapema hata kama umekula chakula kidogo au mara moja kwa siku (improved insulin sensitivity) ambapo hapo awali ulikua unakula sana na kupakua chakula ki