Kufunga Kula Kuna Faida Gani? Kufunga kula kulianza tangu enzi za kale. Hata wanadamu walioshi miaka mingi iliyopita walifunga kwa sababu mbali mbali. Hivi ni nani ambae alisema ya kwamba mwanadamu anatakiwa kula mara tatu kwa siku? Umeshawahi kujiuliza swali hilo? Je, kuna sababu za msingi zinazomfanya mwanadamu ale mara tatu kwa siku, na kuna faida gani endapo atakula pungufu ya hapo? Wagiriki wa kale waliamini ya kwamba kufunga huongeza uwezo wa utambuzi (cognitive ability). Wanafalsafa wengi waliamini ya kwamba kufunga kula ni moja wapo ya tiba katika mwili. Hippocrates ambae ni Baba wa Tiba (father of medicine) aliwaagiza wagonjwa wake wafunge kula ikiwa njia ya kwanza ya tiba kwao kabla ya kuwapa dawa yoyote ile. Hippocrates alisema " To eat when you are sick is to feed your illness" ikiwa na maana ya kwamba " kula chakula wakati ni mgonjwa ni sawa na kuulisha ugonjwa" Mwanafalsafa aitwaye Plutarch pia alisema " Instead of using medicine, better fast
Blog hii ni kwa ajili ya kukusaidia kutatua changamoto za ki afya ambazo zinaweza kutatulika kwa kubadilisha jinsi ya kula na mtindo wa maisha