Gauti (Gout) |
GAUTI NI NINI?
Gauti ni aina ya ugonjwa unaoathiri viungo vya mwili na husababishwa na kuwepo kwa kiasi kikubwa cha tindikali ya urea (excessive Uric Acid) katika damu.
Tindikali ya urea (uric acid) hutokea kama taka mwili inayokuwepo kwenye damu. Tindikali hii hutengenezwa pale ambapo mwili huvunja kemikali ya Purin wakati wa umeng"enyaji wa chakula na hivyo kubaki kwenye damu.
SABABU ZA HATARI KUPATA GAUTI.
- Wanaume hupata Gauti zaidi kuliko wanawake.
- Uzito mkubwa/ unene huongeza hatari ya kupata gauti
- Baadhi ya magonjwa kama vile magonjwa ya moyo, magonjwa ya figo pamoja na kisukari.
- Baadhi ya dawa
- Matumizi ya pombe.
- Vyakula vyenye kiwango kikubwa cha Purine kama vile Nyama nyekundu.
DALILI ZA GAUTI
- Maumivu makali kwenye viungo, haswa kidole kikubwa cha mguu, goti au mguu (ankle)
- Kuvimba vya sehemu ya kiungo
- Sehemu yenye shida kua nyekundu na ya moto.
VYAKULA VINAVYOSAIDIA KUTIBU NA KUZUIA TATIZO LA GAUTI.
NB: kabla ya kuangalia vyakula hivyo, njia rahisi na ya haraka zaidi ni Kupunguza uzito uliozidi, kuacha matummizi ya vitu vya sukari pamoja na kuacha matumizi ya pombe.
- Matunda na mboga za majani: zina kiwango kidogo cha purin na wingi wa Vitamin C.
- Tufaa (Apple): hua na compound maalum iitwayo Malic Acid inayosawazisha kiwango cha tindikali ya Uric kwenye damu.
- Mafuta ya Zeituni (Olive Oil): ina anti oxidants nyingi pamoja na anti inflammation.
- Vyakula vyenye nyuzinyuzi: mfano Oats, Maharage, Parachichi na njegere. Husaidia kuchochea bakteria wazuri wa kwenye tumbo kupunguza inflammation.
- Limao/Ndimu: hua na vitamin C ambayo huyeyusha Uric acid.
- Apple Cider Vinegar (siki ya tufaa): huyeyusha chembe chembe za uric acid kwenye damu endapo utatumia mara 2 au 3 kwa siku, (unatumia kwa kuchanganya kijiko kimoja na kikombe cha maji)
- Maji: husaidia kuyeyusha uric acid iliyozidi.
- Vyakula Vya Vitamin C: mfano machungwa, nanasi na papai. Hupunguza inflammation.
- Tango: ina tabia ya detox inayosaidia kuyeyusha uric acid.
Ipo tiba iliyoandaliwa kwa ajili ya Uric Acid. kwa msaada zaidi juu ya Tiba hiyo tafadhali bonyeza HAPA kisha tuma Ujumbe wa URIC ACID.
Mawasiliano:
- 0753068572 (simu)
- 0621068072 (whatsapp)
Comments
Post a Comment