Erectile Dysfunction |
SABABU ZA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME
Upungufu wa nguvu za kiume, ama kwa jina jingine Erectile Dysfunction (ED) ni ile hali ambayo mwanaume hushindwa kusimamisha uume au kushindwa kusimamisha uume kwa muda mrefu na kuweza kufanya tendo la ndoa. AU ni hali ya mwanaume kushindwa kusimamisha uume kabisa au kushindwa kusimamisha wakati wa kujamiiana hasa baada ya kufika kileleni.
Na hali hii huweza kumtokea mtu yeyote. Kwa kawaida, kila mwanaume huweza kupatwa na hali hii walau mara moja katika maisha yake. Ingawa inapotokea mara kwa mara, basi hilo hua ni tatizo na linahitaji kutatuliwa.
VISABABISHI VYA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME.
- Kisukari: husababisha kusinyaa kwa mishipa ya damu kwenye uume. Hivyo kushindwa kupitisha damu ya kutosha.
- Uvutaji wa Sigara: Nicotine iliyopo kwenye sigara husababisha kusinyaa kwa mishipa ya damu iliyopo kwenye uume. Hivyo kushindwa kuweza kusimamisha uume.
- Magonjwa ya moyo: husababisha mzunguko wa damu kwenye mishiba ya kwenye uume kutokufika vizuri.
- Kiwango kikubwa cha lehemu: lehemu mbaya (bad cholesterol) inapozidi, husababisha uhafifu wa mzunguko wa damu mwilini.
- Saratani ya tezi dume
- kuishi maisha ya kukosa mazoezi
- Upungufu wa homoni ya testosterone: hii ndio homoni ya kiume na ndio inayoshuhulika na tabia au hali ya uwanaume.
- Msongo wa mawazo au sonona.
- Kushindwa kupata usingizi wa kutosha
- Uzito uliopitiliza.
- Matumizi ya pombe kupita kiasi
- Upigaji wa punyeto uliopitiliza.
HOFU YA KUJAMIIANA ( SEXUAL PERFORMANCE ANXIETY)
VITU AMBAVYO WANAUME HUHOFIA ZAIDI.
- kushindwa kusimamisha uume
- Kuendelea kusimamisha hata baada ya mchezo wa kwanza
- Kushindwa kumridhisha mwenzi wake
- Uumw kua mdogo
- Kuhofia pengine ex wa mwenzi wake alikua bora zaidi kitandani kuliko yeye
- Kuwahi kumwaga
- Kuhofia jinsi mwili wako unavyoonekana. (haswa unapojifananisha na watu flani wanaofanya mazoezi na kunyanyua vyuma)
Ieleweke ya kwamba, chanzo kikubwa zaidi cha Sexual Performance Anxiety ni Uangaliaji wa Video za Ngono. (Pornography).
JINSI YA KUONDOKANA NA HOFU YA KUJAMIIANA (SEXUAL PERFORMANCE ANXIETY)
- Punguza na ikiwezekana acha kuangalia video za ngono (pornography): unaweza kua na mpenzi na kufurahia company yake badala ya kukaa mwenyewe na kuangalia porn.
- Fanya sana mazoezi
- Tafuta mtu unaemuamini na uongee nae kuhusiana na changamoto hii.
- Furahia tendo la ndoa na mwenzi wako: jitahidi kuongea nae na muwe marafiki, muone ni mambo gani ambayo yatasaidia wewe kufurahia tendo la ndoa na mwenzi wako.
- Usikimbilie kumaliza tendo, chukua muda (foreplay) kabla ya kuingiza uume kwenye uke.
- Kua na mtindo mzuri wa kula pamoja na maisha.
- Punguza matumizi ya pombe na sigara.
MADHARA YA KUPIGA PUNYETO KUPITA KIASI.
- Hupelekea Uume kushindwa kusimama vizuri au usisimame kabisa.
- Hupelekea kushuka kwa homoni za testosteron, ambazo ndio homoni za kiume.
- kuchoka kwa mwili
- Maumivu sehemu za nyonga
- Maumivu ya korodani.
- Uhafifu wa kuona vizuri.
VYAKULA VINAVYOSAIDIA KUZUIA NA KUPONYA TATIZO LA NGUVU ZA KIUME,
- Mboga za majani: zina wingi wa madini ya Zinc ambayo husaidia kuongeza kiwango cha testosterone pamoja na hamu ya kufanya tendo (libido)
- Jamii ya mbegu (Nuts): kama vile Mlozi na karanga ambazo zina kiwango kikubwa cha Vitamin E ambayo husaidia kua na mishipa yenye nguvu. (ni vyema kutumia za kuchemshwa na sio kukaangwa)
- Tikitimaji: lina wingi wa Vitamin A pamoja na Vitamin C, pamoja na Citrulline (amino acid ambayo husaidia mishipa pamoja na kuimarisha tishu zinazosaidia uume kudinda. Citrulline ipo kwenye ule weupe wa kwenye tikiti kabla ya kufika kwenye nyama)
- kuku, samaki salmoni, kondoo, ng,ombe na bata mzinga: wana kiwango kikubwa cha madini ya zinc.
- Kitunguu Swaumu: wingi wa Hydrogen Sulfide pamoja na akkicin. Hydrogen Sulfide husaidia mishipa kua imara na Allicin huongeza mzunguko wa damu kwenye mishipa. Hivyo damu kufika vizuri kwenye Uume.
VYAKULA VINAVYOONGEZA HAMU YA TENDO LA NDOA
- Kahawa: inaongeza kimetaboliki pamoja na msukumo wa damu.
- Chaza (Oysters): wingi wa zinc pamoja na Vitamin B6 ambazo huongeza kiwango cha testosteron
- Pilipili: hutanua mishipa ya damu na kuzalishwa kwa endorphins inayopelekea kuongezeka kwa mzunguko wa damu.
- Ndizi Mbivu: zina wingi wa Potassium kwa ajili ya kuwezesha ufanisi wa msukumo wa damu.
- Salmon fish: ana wingi wa Omega 3 inayowezesha mishipa ya damu kutokua na hali ya kuganda, hivyo damu kuzunguka kwa urahisi katika mishipa muhimu.
- Mvinyo mwekundu: ina Resveratrol inayosaidia mzunguko kwenye mishipa mikubwa. (tofauti na viagra ambayo hufanya kazi kwenye mishipa midogo)
- Spinach: wingi wa madini ya Zinc
- Tende: wingi wa madini chuma pamoja na potassium.
- Chocolate nyeusi: Cacao ndani yake hufanya uzalishwaji wa endorhins za kutosha ndani ya mwili, Hivyo kuongeza hamu.
- Mboga ya Arugula: huzuia chembe za uchafu zinazosababisha kupungua kwa hamu ya tendo
- Asali: husaidia kuweka uwiano wa homoni za Estrogen pamoja na Testosterone.
- Parachichi: zina wingi wa Vitamin E ambayo huleta hali ya ujana pamoja na nguvu.
- Haradali: huongeza mzunguko wa damu na kuleta hali ya kuweza kusimamisha uume kwa muda mrefu.
- Mdalasini: huzalisha joto mwilini, hivyo kuongeza hamu ya kufanya tendo.
VYAKULA VINAVYOSAIDIA KUONGEZA KIWANGO CHA TESTOSTERONE
- Kitunguu swaumu: kina Diallyldisulfide inayoongeza testicular weight
- Maharage: yana zinc inayosaidia kuongeza testosterone. Zinc huzuia aromatase ambayo ni enzyme inayogeuza testosterone kua estrogen.
- Vitamin A: hupatikana kwenye karoti, viazi vitamu, cantaloupe, mayai n.k
- Nyama (beef): ina madini ya Zinc, Chuma, Protini pamoja na Magnesium. (ila utumie kwa kiasi kidogo)
- Vitamin D: hupatikana kwenye Uyoga, Salmoni pamoja na maziwa.
VYAKULA VINAVYOONGEZA KIWANGO CHA SHAHAWA NA UWEZO WA KUTUNGISHA MIMBA.
- Chaza
- Chocolate nyeusi
- Mmea wa Maca
- Ndizi
- Asparagus
- Mbegu za Walnuts
- Squash
- Ginseng
- Kitunguu swaumu
- Mbegu za maboga
- Vyakula vyekundu kama vile nyanya.
Kwa mawasiliano zaidi
Comments
Post a Comment