Mfungo wa chakula |
JINSI YA KUFANYA DIET KAMA UPO KWENYE MFUNGO.
Zipo sababu nyingi sana ambazo hufanya watu wafunge kula. Kuna sababu za Kiimani (kwaresma, Ramadan au kua na mfungo wa maombi maalum), kuna wale ambao hufunga kwa sababu nyingine lakini kuu zikiwa ni za kiimani.
Sasa watu wengi hudhania ya kwamba kama wanafanya diet basi kuna ratiba maalum kwa ajili ya msimu wa Mfungo mfano Ramadan, Kwaresma au nyinginezo.
Lakini hamna jambo llolote linalobadilika wakati wa mfungo huo zaidi tu ya kubadilika kwa muda wa kula.
JINSI YA KULA AU RATIBA YA KUTUMIA
Kama unafwata Diet yoyote ile, basi bila shaka kuna vyakula hua unatumia kwa ajili ya kukusaidia kuweza kupungua.
Kama umefunga. (wengi hufunga mchana na kufungua jioni), hamna kinachobadilika zaidi tu ya muda wa kula.
Angalia ratiba yako kwa siku usika unakula nini, Basi kile cha asubuhi unaweza Kukitumia Kama daku (kwa wale wa Ramadan), na kisha jioni wakati wa kufungua, kilichopo kwenye ratiba yako ya usiku ndio ukatumia kama Ftari au kufungua.
Lakini sio lazima utumie kilichopo kwenye ratiba ya siku hiyo, kikubwa ni Kutumia vitu ambavyo vipo kwenye mwongozo wa Diet yako. Hivyo chochote kile ambacho kipo kwenye mwongozo unaweza kutumia bila shida yoyote ile.
Hamna kinachobadilika, bali tu muda wa kula ndio ambao unabadilika.
Kwa msaada zaidi
Comments
Post a Comment