VIRUTUBISHO 6 VYENYE AFYA
Japokua, kila tunachokula au kunywa, hytofautiana virutubisho vinavyopatikana. Kuna ambavyo vimejaa virutubisho, na kuna ambavyo havina virutubisho na hivyo kua havina faida kwenye mwili wa mwanadamu ingawa vinaonekana kua na ladha nzuri.
VIRUTUBISHO 6 VYENYE AFYA NA VYAKULA VYAKE.
1. NYUZI NYUZI
Nyuzi nyuzi husaidia sana kuratibu uzito wa mwili, kupunguza hatari za kisukari na lehemu (cholesterol) kwenye damu, Pia kupunguza athari za magonjwa ya moyo.
Nyuzi zisizo yeyuka husaidia sana kuweka mfumo wa chakula na msukumo uende kwa urahisi.
vyakula Vyenye nyuzi nyuzi ni kama vile Njegere, karoti, maharage mabichi, cauliflower, viazi vitamu, matunda
2. VITAMIN A
Husaidia sana kuona kwa macho na kukinga mwili dhidi ya magonjwa ya kuambukiza. Pia husaidia kuwezesha nyama za mifupa, ngozi na meno kuwa na afya nzuri.
Vyakula vyenye Vitamin A ni kama vile; Matunda yenye rangi ya pink, brokoli, spinachi, aprikoti, viazi vitamu, mboga za majani, mayai n.k
3. VITAMIN C
Husaidia sana kuimarisha mfumo wa mifupa kama meno, mifupa, mifupa laini (cartilage). Husaidia kuponya vidonda na kujenga protini na mishipa ya damu na ngozi katika kidonda.
Husaidia pia kunyinywa kwa madini ya chuma, hulinda miili yetu dhidi ya chembechembe zinazotokana na kuunguzwa kwa chakula mwilini (free radicals)
Vyakula vyenye Vitamin C ni kama vile; Cauliflower, kabichi, viazi vitamu, brokoli, maembe, matikiti maji, mananasi, mapapai, machungwa, zabibu na hoho nyekundu.
4. MADINI YA CHUMA
Husaidia mishipa ya damu kuhifadhi hewa ya oksijeni na kuitumia. Madini ya chuma hupatikana kwenye chembechembe nyekundu za damu ambayo husafirisha oksijeni mwilini.
Vyakula ni vyenye madini ya chuma ni kama vile; Maboga, spinachi, maharage, mboga za majani, nyama nyekundu, maini (ila epuka wakati wa ujauzito), n.k
5. ANTIOXIDANTI (ANTI OXIDANTS)
Hulinda mwili dhidi ya chembechembe (free radicals) zinazotolewa wakati wa kusagwa chakula mwilini ambapo huungana nazo na kuondoa uharibifu wake.
Free radicals husababisha kupungua kwa nguvu za kioo cha macho, maumivu ya viungo (arthritis), uharibufu wa mishipa ya ubongo (nerves) inayoleta ugonjwa wa kupoteza kumbukumbu (Alzheimer), zinaongeza hatari ya magonjwa ya moyo, zinaharakisha uzee na kusababisha magonjwa ya saratani kwa kuharibu seli za DNA.
NB: DNA (Deoxyribo Nucleic Acid) hutoa maelekezo ya urithi wa Tabia au umbile katika kizazi.
6. OMEGA-3
Omega-3 zinazotokana na samaki hupatikana kwenye dagaa, jodari, sangara na vibua. Pia mayai yana kiwango kidogo cha Omega-3
Mpaka kufikia hapo, utakua umeelewa kitu kuhusu virutubisho ambavyo vinafaida kubwa mwilini. Na utakua umejua ni vyakula gani utumie ili kufaidika kwa kupata virutubisho hivyo.
By Samuel Macha (FIT BY WAYNE)
Comments
Post a Comment