kwa nini unaongezeka uzito. |
SABABU 15 KWA NINI UNAONGEZEKA UZITO
yawezekana umekua ukifanya mazoezi na kutafuta njia kadhaa za kuweza kupunguza uzito ambao umezidi, ila mara nyingi unakwama na hufikii malengo yako.
Huenda ni kwa sababu hujazijua sababu hizi zinazosababisha kuongezeka kwa uzito.
1. KUTOKUPATA USINGIZI WA KUTOSHA
Haswa wakati wa usiku, hii husababisha kitu kinaitwa LOWER RESTING METABOLIC RATE
2. MVURUGIKO WA HOMONI (HORMONAL IMBALANCE)
3. WATER RETENTION (MAJI YANAYOBAKI MWILINI BILA KUTOKA)
Mwili wako unapohifadhi maji mwilini bila kutumika, utagundua ya kwamba uzito unaongezeka. Hii ni kwa sababu maji pia yana uzito, hivyo yanavyozidi kua mengi mwilini, na uzito unaongezeka. Moja ya sababu zinazopelekea hali hii ni utumiaji wa chumvi nyingi, pia baadhi ya dawa, kubadilika kwa homoni, au baadhi ya hali za ki afya.
4. STRESS/DEPRESSION (MSONGO WA MAWAZO/SONONA)
Unapokua katika hali hii, mwili wako hua unaachilia homoni ya cortisol unapokua na stress kwa muda mrefu pamoja na adrenaline. unapokua na mashaka au wasiwasi, hizi homoni hujiandaa kuweka mwili wako katika hali ya SURVIVAL MODE, inayopelekea mwili kutunza mafuta.
5. KULA ZAIDI YA KIWANGO CHA KAWAIDA
Hata kama chakula ni chenye afya, unatakiwa ule kiasi cha kawaida kitakachokufanya ushibe na sio kuvimbiwa. Yawezekana vyakula unavyokula vina calorie chache, ila ukumbuke ya kwamba CHEMBE NA CHEMBE MKATE HUWA.
6. KUTANUKA AU KWA MISULI
Kuna baadhi ya mazoezi hufanya misuli itanuke zaidi, na kutanuka kwa misuli maana yake hata uzito unaongezeka.
7. MARA BAADA YA KUACHA SIGARA
Mara nyingi mtu anapoamua kuachana na sigara, anaweza kuona anaongezeka mwili au uzito kidogo, Hivyo ni vyema mtu huyu akatumia mboga mboga kwa wingi pamoja na maji.
8. KUCHELEWA KULA MLO WA JIONI.
Unapokula chakula chini ya masaa matatu kabla ya kwenda kulala, mwili hautapata muda wa kuyeyusha chakula tumboni pamoja na zile calorie ambazo umeingiza.
9. USAFI MBOVU WA KINYWA.
Mwili wa mwanadamu umeunganika katika maeneo mengi, inapotokea ukapata kichochezi (inflammation) kwenye fizi, basi na sehemu nyingine za mwili zinakua kama zimepata hiyo shida na kuanza kuhifadhi mafuta.
10. KUTUMIA ZAIDI VYAKULA VYA KUNUNUA KULIKO KUANDAA NYUMBANI
Mara nyingi vyakula vya kununua kwa asilimia kubwa sio rafiki na huongeza uzito, hivyo unapokula kila siku, HABA NA HABA HUJAZA KIBABA.
11. KULA CHAKULA KINGI BAADA YA MAZOEZI
Unaweza usijue ni kiasi gani cha calorie umetumia wakati wa mazoezi, na pia usijue kiwango cha calorie utakachoingiza punde tu utakapokula chakula hicho
12. UKOSEFU WA MAJI MWILINI (DEHYDRATION)
Itapunguza ufanisi wa kimetaboliki na jinsi mwili wako unavyochoma mafuta. Hii itakufanya calorie unazoingiza ziwe nyingi kuliko unazozitoa.
13. UTUMIAJI WA JUISI NA VINYWAJI (ISIPOKUA MAJI)
Hali hii hupelekea kuingiza calorie nyingi zaidi kwa siku kuliko mwili unavyotumia, kwa sababau ni rahisi zaidi kunywa kuliko kunywa.
14. UCHAFUZI WA HEWA
Tafiti zinaonyesha ya kwamba watu wanaoishi maeneno ambayo kuna uchafuzi mkubwa wa hewa hujikuta na uzito mkubwa zaidi na hatari ya magonjwa ya moyo kuliko wale ambao wanaishi sehemu ambazo hazina uchafuzi huo.
Ndio maana katika program nilizotoa hapo awali, tulianza na Detox kwanza kwa ajili ya kutoa taka mwili kutoka kwenye miili yetu.
15. KUISHI BILA KUJUA UZITO WAKO MARA KWA MARA
Wewe una kilo ngapi??? Watu wengi ukiwauliza swali hili, watakujibu hivi... MARA YA MWISHO ILIKUA..... maana yake hana uhakika sasa hivi anazo ngapi. Kujua uzito wako mara kwa mara itakusaidia kujua wapi upunguze na wapi uache. kwa sababu uzito ukiongezeka taratibu hutajua, ni siku tu itatokea mtu anakwambia... FLANI UMENENEPA... na wewe unaanza kushangaa.
Comments
Post a Comment