Skip to main content

ASALI NA LIMAO KATIKA KUPUNGUZA UZITO

 

Asali na Limao

ASALI NA LIMAO KATIKA KUPUNGUZA UZITO.

Kuna mengi sana yanasemwa kuhusiana na asali. Wengine husema asali huongeza uzito kama sukari, na wengine husema ya kwamba asali hupunguza uzito. lakini je, ukweli haswa ni upi?

Kwa kawaida, ni kweli ya kwamba asali ina calories nyingi. Asali ina calorie 304 katika kila gram 100. Hivyo ni kiasi kikubwa.

lakini vile vile, Asali ikitumika katika mchanganyiko wake maalum, inaweza kukusaidia kupunguza unene, uzito pamoja na kitambi au nyama zembe endapo utatumia mara kwa mara. (IFAHAMIKE YA KWAMBA, HUWEZI KUPUNGUA UZITO KAMA HUBADILISHI MTINDO WAKO WA KULA NA MAISHA)

Hapa tutatumia mchanganyiko maalum kwa ajili ya kukusaidia kuweza kupunguza uzito, kitambi pamoja na unene kwa ujumla. Japokua mchanganyiko huu una faida nyingine nyingi, ila kwa sasa nitaelezea kuhusiana na uzito.

MAHITAJI YA MCHANGANYIKO WAKO

  • Asali mbichi kijiko kimoja cha chai
  • Maji ya vuguvugu kikombe 1
  • Vijiko 2 vya maji ya limao

JINSI YA KUTENGENEZA

  • Chukua limao lako kisha likate na ukamulie kwenye chombo chochote
  • Weka maji ya vuguvugu kwenye kikombe chako 
  • Chota maji ya limao ambayo ulishakamulia kwenye kile chombo, vijiko 2 tu vya maji ya limao, na kisha uchanganye kwenye kikombe chenye maji ya vuguvugu
  • Weka Asali mbichi kijiko kimoja cha chai kwenye mchanganyiko wako
  • Koroga mchanganyiko wako ili uchanganyike vizuri.

MATUMIZI

  • Kunya mchanganyiko wako asubuhi kabla ya kula kitu chochote.
  • Au unaweza kutumia mchanganyiko wako kila baada ya mlo mkubwa kama unaweza.

MAMBO YA KUZINGATIA

  • Zingatia ulaji mzuri (kwa wale ambao mnafwata ratiba ya PREMIUM mna faida kubwa zaidi)
  • Endapo utatumia mchanganyiko huu, lakini bado unakula vibaya, hautapata matokeo mazuri na kazi yote itakua ni bure.
By SAMUEL MACHA, FIT BY WAYNE

CONTACTS:
mobile: 0753068572
whatsapp: 0621068072 Au bonyeza WHATSAPP

Comments

Popular posts from this blog

DETOX YA SIKU 7. HATUA YA KWANZA KUPUNGUZA UNENE

  HATUA YA KWANZA KUPUNGUZA UNENE. Uzito Unaotakiwa kua nao Kulingana na Urefu Pamoja na Jinsia UREFU (CM) UREFU (FT & INCH) UZITO (KG)       MWANAUME MWANAMKE 147 4' 10" - 45-59 150 4' 11" - 45-60 152 5' 0" - 46-62 155 5' 1" 55-66 47-63 157 5' 2" 56-67 49-65 160 5' 3" 57-68 50-67 162 5' 4" 58-70 51-69 165 5' 5" 59-72 53-70 167 5' 6" 60-74 54-72 170 5' 7" 61-75 55-74 172 5' 8" 62-77

Hormonal Imbalance, Visababishi na Tiba yake

  Hormonal Imbalance HORMONAL IMBALANCE    Hormonal imbalance ama kwa Kiswahili ni mvurugiko wa kichochezi (hormone). Mara nyingi huwakumba wanawake Zaidi, ingawa hata wanaume wanaweza kua na tatizo hili. na kusababisha kiwango kidogo sana au kikubwa sana cha hormone au kichochezi chochote kutokukaa sawa.  NINI HUSABABISHA HORMONAL IMBALANCE  1️⃣Ulaji Mbovu wa chakula 2️⃣Unene (uzito uliopitiliza) 3️⃣Matumizi ya dawa za uzazi wa mpango.  4️⃣Stress na msongo wa mawazo 5️⃣kisukari 6️⃣Hyperglycemia (uzalishwaji wa kuzidi wa glucagon) 7️⃣Hypoglycemia (insulin kuzalishwa nyingi kuliko glucose kwenye damu) 8️⃣Saratani pamoja na vimbe kwenye via vya kizazi.  DALILI ZA HORMONAL IMBALANCE  1️⃣Kupungua kwa hamu ya tendo la ndoa 2️⃣Kutokushika mimba (infertility) 3️⃣Kutokua na uwezo wa kusimamisha uume 4️⃣Mbegu za uzazi kuwa chache (low sperm count) 5️⃣Uke kua mkavu (vaginal dryness) 6️⃣Kubadilika badilika kwa mzunguko wa hedhi au maumivu makali 7️⃣Kutokupata usingizi vizuri 8️⃣Kuongezeka uzito

BAWASIRI NA JINSI YA KUITIBU KWA NJIA ZA ASILI

 BAWASIRI NA JINSI YA KUITIBU KWA NJIA ZA ASILI.   💊💊💊💊💊💊💊💊💊💊💊💊💊   BAWASIRI NI NINI?   Bawasiri (kikundu, future, puru au mjiko ) ni hali ya kutuna kwa mishipa ya damu katika mfereji wa sehemu ya haja kubwa (anus). Kuna aina mbili za Bawasiri;   1. Bawasiri za ndani ( internal haemorroids )   2. Bawasiri za nje ( external haemorroids )  Bawasiri za ndani hua na dalili ya kupata kinyesi kilichokua na damu,  bawasiri za nje hua na dalili ya maumivu makali wakati wa kujisaidia pamoja na kinyama kutoka kwa nje.  NINI VISABABISHI VYA BAWASIRI?   1️⃣Historia ya familia, mara nyingi baadhi ya familia hukumbwa na changamoto hii. Na hua watu wa familia hiyo husika wanakua na hili tatizo. 2️⃣Kupata choo kigumu mara kwa mara husababisha mtu kutumia nguvu nyingi (straining) ambayo husababisha bawasiri kutokea. 3️⃣Unene (uzito uliopitiliza) hua ni kisababishi cha bawasiri kwa sababu ya kuongezeka kwa Rectal Vein Pressure. 4️⃣Kukaa sehemu moja kwa muda mrefu au kutokufanya mazoezi. (sed