wastani wa kupungua |
WASTANI WA KUPUNGUA KWA MWEZI.
Bila shaka kama una uzito mkubwa, umeshawahi kutamani ungepunguza kilo nyingi sana ndani ya muda mfupi.
Lakini je, unatakiwa kupungua wastani wa kilo ngapi kwa mwezi?
Pia umeshawahi kuona ya kwamba kuna mtu anapungua haraka sana ndani ya muda mfupi, lakini baada ya muda mfupi ananenepa tena, na pengine Zaidi ya mwanzo. Na vile vile kuna ambae anapungua kwa mwendo wa kawaida, lakini akishapungua na kufikia uzito sahihi, basi hanenepi tena. Au hanenepi kwa urahisi.
JE, NI WASTANI WA KILO NGAPI UNATAKIWA KUPUNGUA KWA MWEZI?
Wataalam wa afya wanashauri ya kwamba upungue uzito kwa spidi ambayo ni ya wastani au kawaida, yaani sio ya haraka sana kupita kiasi. Hii itakusaidia kua na uzito sahihi kwa muda mrefu Zaidi.
Kupungua uzito hutegemea UMRI , JINSIA , UCHANGAMFU WA MTU (PHYSICAL ACTIVITY LEVEL/MAZOEZI) pamoja na MATOKEO YA DAWA/DOZI MBALI MBALI . Hivyo kila mtu huenda kwa spidi yake.
Kwa kawaida, ni afya Zaidi kupungua kuanzia kilo 2 hadi kilo 4 kwa mwezi. Yaani sawa na asilimia 5 hadi 10 ya uzito wako kwa ujumla. (Dr Elizabeth Lowden, bariatric endocrinologist).
Pia unaweza kupungua hadi kilo 6, wengine huweza kwenda hata 8. Ni kawaida.
Katika tumbo pia kwa kufwata ratiba hii niliyotoa, ni wastani wa sentimita 4cm kwa mwezi. Ingawa inaweza kua kubwa Zaidi au kua pungufu kidogo. Hivyo unaweza kujiona ya kwamba haupungui kilo, ila ukashangaa baadhi ya nguo ambazo ulikua huwezi kuzivaa sasa unaweza kuvaa. Ni kwa sababu ya cm katika tumbo pia hupungua.
Kwa kawaida, wiki ya kwanza unaweza kupungua kilo nyingi, na cm nyingi. Hii ni hali ya kawaida kabisa. Kitaalam kuna kitu tunaita WATER RETENTION , yaani maji ambayo yalikua yamezidi mwilini.
Zipo sababu nyingi zinazosababisha maji kuzidi mwilini, moja wapo ikiwa matumizi ya chumvi nyingi. Ndio maana wakati unafanya detox, uliweza kupungua kilo nyingi kwa wiki moja. (japo sio kwa wote, inategemea na kiasi cha maji mtu alichokua nacho). Na kwa kua maji yana uzito, ndio maana yakipungua baada ya figo kufanya kazi, unaona na kilo zinapungua.
Baada ya maji hayo kupungua, sasa unaanza kupungua taratibu Zaidi ya mwanzo, ambapo hapa sasa ndio muda ambao mwili wako unajitengeneza kua FIT Zaidi.
NI KWA NINI SIO VIZURI KUPUNGUA KILO NYINGI KWA MUDA MFUPI?
🍏Ukipungua kilo nyingi sana ndani ya muda mfupi, mwili wako utapigana ili uweze kurudisha kilo hizo. (Body's defence mechanism), metabolism yako itapungua na hormones zitabadilisha jinsi zinavyofanya kazi ili kuongeza hamu ya kula na kufanya kuchoma mafuta kwa kiwango kidogo sana.
🍏Lakini pia, ukipungua kwa spidi kubwa sana, utapoteza kiasi cha misuli yako, kitaalam tunaita LEAN MUSCLE MASS . Haswa kama sio mtu wa kufanya mazoezi.
NINI UFANYE WAKATI UPO KWENYE SAFARI YA KUPUNGUA.
🍏 Jiandae kufanikiwa: ni vyema kujiandaa kiakili pamoja na kimahitaji ili uweze kufika katika safari yako ya kupungua. Kamwe usisahau lile lengo lako.
🍏 Jiandae kwa changamoto na kukabiliana nazo: safari hii ni ngumu, lakini inawezekana. Kuna muda unatamani kula vibaya (vyakula visivyofaa), kuna muda unaenda kwa watu na ratiba yao ni tofauti na yako, pamoja na changamoto nyingine nyingi. Pia kumbuka kuna muda utafikia ile WEIGHT LOSS PLATEAU . Ni vyema kuyafahamu haya yote ili usije ukakata tamaa. Kumbuka, YOU ARE WHAT YOU EAT. Yaani wewe ulivyo ni jinsi ya unavyokula.
🍏 Fahamu vitu vya msingi katika kupungua: kula vizuri (kama nilivyoelekeza), kua mchangamfu (physical activity) na kupata usingizi wa kutosha. Kamwe usisahau ya kwamba, kila unachokula, ni ama unapambana na magonjwa, au unakuza (unafuga) ugonjwa na matatizo mengine ya afya. Hivyo ni vyema kula vizuri.
Kumbuka ya kwamba, mwongozo wa jinsi ya kula niliokupa, sio kwamba ni kitu flani special, au kwamba ni diet flani special, la hasha. Bali ni mtindo wa maisha kama unapenda kua na afya nzuri. Kua na afya nzuri kunaendana sambamba na kua na uzito sahihi.
By SAMUEL MACHA
FIT BY WAYNE.
Comments
Post a Comment