Skip to main content

VYAKULA VIZURI KUTUMIA WAKATI WA COVID-19

 

COVID-19 FOODS
Uwepo wa kirusi cha Corona, dunia nzima inapambana katika kujilinda na maambukizi haya. Hivyo ni vyema kufwata ushauri wa wataalam katika kujikinga na kuwakinga wengine dhidi ya maambukizi haya.

kitu kikubwa zaidi ni kuhakikisha kua kinga ya mwili iko imara. Na unaweza kuimarisha kinga ya mwili kwa kutumia vyakula vinavyosaidia kuimarisha kinga ya mwili. Kinga ya mwili inapoimarika, basi inakua na uwezo wa kupambana na maambukizi yoyote yale yasiweze kukupata au kukuletea athari kubwa.

VYAKULA VINAVYOONGEZA KINGA YA MWILI

  1. MANJANO (TUMERIC): ina compound ambayo ni anti-inflammatory iitwayo curcumin ambayo hua inahamasisha uzalishwaji wa T cells ambazo ndio cell zinazopigania afya yako kwenye kinga ya mwili.
  2. NYANYA: ni nzuri kuzila haswa unapoumwa kwa sababu ya wingi wa Vitamin C. nyanya moja ina zaidi ya mg 16 za Vitamin C ambayo ni muhimu sana kwenye kinga yako ya mwili. (ili iwe rahisi kuila yenyewe, unaweza kuitumia kwenye kachumbari)
  3. SAMAKI WA SAMONI (SALMNON FISH): wana wingi wa madini ya Zinc ambayo hua inasaidia kupunguza dalili za mafua (common cold)
  4. PAPAI: zina wingi wa Vitamin C, pia zina enzyme inayoitwa Papain ambayo ina anti-inflammatory effect. Hivyo inasaidia kupambana na maambukizi. Pia papai lina Pottasium, Vitamin B pamoja na Folate (Vitamin B9) ambazo zinasaidia kuimarisha cell za mwili.
  5. GREEN TEA: ukiachilia na faida zake katika kupunguza uzito, pia inasaidia kuongeza nguvu na kuimarisha kinga ya mwili kwa sababu ya uwepo wa flavanoid  ambayo ni antioxidant na pia anti-inflammatory. Pia ina anti-oxidant iitwayo catechin ambayo ni antibacterial na antiviral (yaani uwezo wa kupambana na bacteria pamoja na virusi)
  6. UYOGA: husaidia sana kuongeza kinga ya mwili kwa kuongeza wingi wa T-cells. 
  7. CHAZA (OYSTERS): chaza huchangia 190% ya selenium, 40% madini ya chuma pamoja na 20% ya Vitamin C. Pia zina Zinc pamoja na Vitamin A, Ambazo zote kwa pamoja husaidia kuimarisha kinga ya mwili.
  8. MTINDI (LOW FAT YOGURT): yana gram 11 za Protini, calorie 250 na milligram 400 za Calcium kwa kila kikombe kimoja cha mtindi. Pia Vitamin B12, Vitamin D pamoja na Vitamin B2. Kipekee kabisa Mtindi una probiotics (bacteria wazuri) ambao hufanya kinga ya mwili kua juu.
  9. SPINACH: zina wingi wa Folate, Vitamin A, Vitamin C, Fiber. Magnesium pamoja na madini ya chuma. Vyote kwa pamoja husaidia katika DNA reparing ambayo hufanya kinga ya mwili iwe vizuri. Spinach huliwa mbichi, au kama ukipika, basi inatakiwa zisiive sana ili kuweza kupata virutubisho vyote.
  10. VIAZI VITAMU: vina wingi wa Beta carotene, ambayo husaidia kuongeza kinga ya mwili kwa kusaidia uzalishwaji wa chembechembe nyeupe za damu (white blood cells) ambazo zinapambana na bacteria pamoja na virusi. (ni vizuri kutumia vikiwa vimechemshwa, kuokwa au kuchomwa badala ya kukaanga.)
  11. VITUNGUU SWAUMU: vinasaidia sana kuongeza kinga ya mwili, pia vina tabia ya ki anti-biotic.
  12. MBEGU ZA MLOZI (ALMONDS): zina wingi wa Vitamin E ambapo ni nzuri kupambana na mafua au kikohozi. ila ni vyema kutumia kwa kiasi, kwani zina calorie nyingi.
  13. TUNDA LA KIWI: zina wingi wa vitamin C, Vitamin K, Potassium pamoja na Folate. ambazo ni anti oxidants na kusaidia kupambana na maambukizi.
  14. MBEGU ZA ALIZETI: zina wingi wa Vitamin E, Vitamin B6, Magnesium na Phosphorus ambazo zote husaidia kuongeza kinga ya mwili.
  15. MATUNDA YA CITRUS (MACHUNGWA, NDIMU, LIMAO, GRAPEFRUIT N.K): yana wingi wa Vitamin C ambayo ni muhumu katika uzalishwaji wa white blood cells zinazopambana na maambukizi mbalimbali.
  16. POULTRY (KUKU, BATA, TURKEY N.K): wingi wa Vitamin B6 inayosaidia katika uzalishwaji wa Red Blood Cells pamoja na kuweka kinga ya mwili sawa kwa ujumla. Supu ya kuku ni nzuri zaidi kuliko akikaangwa.

Pamoja na mambo mengine mengi ambayo unaweza kufanya ili kuweka sawa kinga yako ya mwili. Sio tu kufanya, bali kuna ambayo unatakiwa kuacha kufanya ili kuendelea kuweka sawa kinga yako ya mwili.

Kua mtu wa mazoezi mara kwa mara, kunywa maji mengi, pata muda mzuri wa kulala na kupunmzika. Punguza matumizi ya sigara na Pombe, jitahidi kua na uzito sahihi (kupunguza uzito uliozidi) ili kuweza kua na kinga bora ya mwili)

By SAMUEL MACHA
FIT BY WAYNE.

Comments

Post a Comment

Popular posts from this blog

DETOX YA SIKU 7. HATUA YA KWANZA KUPUNGUZA UNENE

  HATUA YA KWANZA KUPUNGUZA UNENE. Uzito Unaotakiwa kua nao Kulingana na Urefu Pamoja na Jinsia UREFU (CM) UREFU (FT & INCH) UZITO (KG)       MWANAUME MWANAMKE 147 4' 10" - 45-59 150 4' 11" - 45-60 152 5' 0" - 46-62 155 5' 1" 55-66 47-63 157 5' 2" 56-67 49-65 160 5' 3" 57-68 50-67 162 5' 4" 58-70 51-69 165 5' 5" 59-72 53-70 167 5' 6" 60-74 54-72 170 5' 7" 61-75 55-74 172 5' 8" 62-77 ...

BAWASIRI NA JINSI YA KUITIBU KWA NJIA ZA ASILI

 BAWASIRI NA JINSI YA KUITIBU KWA NJIA ZA ASILI.   💊💊💊💊💊💊💊💊💊💊💊💊💊   BAWASIRI NI NINI?   Bawasiri (kikundu, future, puru au mjiko ) ni hali ya kutuna kwa mishipa ya damu katika mfereji wa sehemu ya haja kubwa (anus). Kuna aina mbili za Bawasiri;   1. Bawasiri za ndani ( internal haemorroids )   2. Bawasiri za nje ( external haemorroids )  Bawasiri za ndani hua na dalili ya kupata kinyesi kilichokua na damu,  bawasiri za nje hua na dalili ya maumivu makali wakati wa kujisaidia pamoja na kinyama kutoka kwa nje.  NINI VISABABISHI VYA BAWASIRI?   1️⃣Historia ya familia, mara nyingi baadhi ya familia hukumbwa na changamoto hii. Na hua watu wa familia hiyo husika wanakua na hili tatizo. 2️⃣Kupata choo kigumu mara kwa mara husababisha mtu kutumia nguvu nyingi (straining) ambayo husababisha bawasiri kutokea. 3️⃣Unene (uzito uliopitiliza) hua ni kisababishi cha bawasiri kwa sababu ya kuongezeka kwa Rectal Vein Pressure. 4️⃣Ku...

CALORIE ZA VYAKULA VYA TANZANIA

 CALORIES ZA VYAKULA TANZANIA   NINI MAANA YA CALORIE?    Calorie ni kiasi cha nishati kinachohitajika ili kuongeza joto la gramu moja ya maji (°C). Kwa lugha nyepesi, calorie katika chakula hutoa nishati (energy) kwa njia ya joto ili miili yetu iweze kufanya kazi. Hii ni kwa sababu miili yetu huhifadhi na kuchoma calorie kama mafuta.  UHUSIANO WA CALORIE NA UZITO WA MWILI.  Kwa kawaida, kila chakula kina kiwango chake cha calorie. Hivyo unapokula chakula, unaingiza mwilini calorie kadhaa, na mwili wako pia unatumia calorie katika kuweka uhai. Lakini unapokula chakula, unaingiza calorie mwilini. Na mwili wako pia unatumia calorie kama nishati. Hivyo unapokula calorie nyingi kuliko mwili unavyoweza kutumia, zinahifadhiwa kama mafuta na utaongezeka uzito. Unapotumia calorie nyingi kuliko unavyoingiza mwilini, unapungua uzito. Na ukitumia kiasi sawa na unachoingiza, basi unabaki na uzito ule ule.   MWANADAMU ANAHITAJI WASTANI WA CALORIE NGAPI? ...