USILE VYAKULA HIVI KAMA UNA UMRI WA MIAKA 30 AU ZAIDI
'The doctors of the future will no longer treat the human frame with drugs, but rather will cure and prevent disease with nutrition’ - Thomas Edison.
Lishe ndio kitu kikubwa Zaidi katika kuboresha au kubomoa afya ya mwanadamu. Na kwa kutumia lishe pekee, una uwezo wa kufanya mwili wako uwe na uwezo mkubwa wa kujitibu wenyewe.
Kama una umri (au utakapofikisha umri) wa miaka 30 na Zaidi, basi vyakula hivi jitahidi kuviepuka.
- Pombe : hua ina kalori nyingi sana, na kuanzia umri wa miaka 30 mwili hauwezi tena kuzichoma zote na hivyo kuhifadhiwa kama mafuta na kusababisha kitambi/unene. Pia inabadilisha kiwango cha insulini na kusababisha kua na hamu ya kula vitu vyenye sukari.
- Sukari za kutengenezwa: hizi husababisha mwili wako usitumie kalori zake vizuri na pia huongeza hatari ya saratani. Pia husababisha glucose kuwepo kwa kiwango kikubwa na kupunguza ufanisi wa insulini. Hivyo kusababisha kuongezeka kwa uzito, magonjwa ya moyo na kisukari.
- Caffeine : hii husababisha kuzeeka mapema na pia kusababisha kua na hamu ya kula vitu vya sukari inayopelekea kuongezeka kwa uzito/kitambi.
- Ngano iliyokobolewa : mwili wako unageuza ngano hii kua glucose na hivyo kuhifadhiwa mwilini kama mafuta. Hivyo ni vyema kutumia ngano ambayo haijakobolewa.
- Mtindi ulioongozewa ladha bandia : bila shaka unafahamu yogurt za viwandani zenye ladha ya strawberry, chocolate, vanilla n.k hizi hua na sukari nyingi sana ambayo sio nzuri kwako
- Maziwa : vyakula vitokanavyo na wanyama hua na kiwango kikubwa cha acid. Na maziwa mengi hua yanasafishwa ili kuua vijidudu ambapo hupelekea kuua na virutubisho. (kwa maziwa ya viwandani)
- Vyakula vya kwenye makopo : hivi hua na kiwango kikubwa cha sukari, chumvi na mafuta. Na vyote hivi sio vizuri kwa afya.
- Soda : ina kiwango kikubwa cha sukari ya fructose corn syrup ambayo ni mbaya sana kwa afya kwa sababu yenyewe huenda moja kwa moja kwenye ini na kuhifadhiwa kama mafuta (fat). Pia husababisha mwili usitumie leptin (leptin resistance) ambayo ni hormone inayofanya uwiano wa hamu ya kula na kufanya uwe na kiu ya soda Zaidi au vitu vya sukari. Na hii ndio hupelekea kunenepa Zaidi na kua na kitambi.
THE BEST KEPT SECRET OF MEDICINE IS THAT, THE BODY HEALS ITSELF IF WE CREATE THE RIGHT CONDITIONS.
Imeandikwa na SAMUEL MACHA,
FIT BY WAYNE.
CONTACTS: Mobile 0753068572, whatsapp WHATSAPP
Mungu akuzidishie umri unasaidia wengi
ReplyDeleteAmina
DeleteHuwa natumia maziwa fresh na mhogo wa kuchemshwakutwa nikisickia njaa huwa nakula parachichi je ninakosea naomba msaada wako
DeleteMungu akuongezee maarifa tuzidi kupata elimu
ReplyDeleteAmen
DeleteAnsante Kwa kutupatia maarifa
ReplyDeletekaribu sana
DeleteAsante sana kwa masomo mazuri mungu atakulipa zaidi
DeleteHapo Kwenye maziwa,ugonjwa 🤔🤔🤔
ReplyDeleteHakuna linaloshindikana endapo utaweka nia
DeleteAsante kwa darsa mungu akulipe hitaj lako
ReplyDeleteAmen, hata kwako pia
Deleteahsante Sana sijawahi kujutia kukujua
ReplyDeleteNashukuru sana kwa hilo
DeleteAsante Sana Dr.... Binafsi umenisaidia Sana
ReplyDeletekaribu sana
DeleteMm soda nilisha acha hata chai nina muda mrefu sana sijanywa
ReplyDeleteMungu akubariki Mdogo wangu Samwel,,,Sijutii kukufahamu!
ReplyDelete