MLO SAHIHI KULINGANA
NA KUNDI LAKO LA DAMU (BLOOD GROUP)
Kuna msemo unaosema kua ONE
MAN'S FOOD IS ANOTHER MAN'S POISON. Yaani ikiwa inamaanisha kua.
Chakula ambacho kina manufaa kwako, huenda kikawa ni sumu kwa mtu mwingine.
Sasa najua utajiuliza kua kwa nini ipo hivi. Hii ni kwa
sababu sisi tupo vile tulivyo kulingana na kundi la damu tulilo nalo. Damu ni
uhai, damu haielezeki kiurahisi. Lakini ndio inatupa uhai sisi binadamu na
viumbe vingine vyote. Lakini je, kutokana na makundi ya damu tuliyonayo, ni
sahihi kila kundi kula mlo mmoja??
Labda nitoe mfano kidogo; Blood group O wanafanya vizuri sana
wakila protini kama nyama, kwa sababu hawa hua wana acid nyingi tumboni, na
ndio maana Blood Group O wengi wana vidonda vya tumbo.
Lakini blood group A wanafanya vizuri sana kama wakila mboga
za majani. Kwa sababu wakila nyama inawatesa kwenye mmeng'enyo wa chakula na huhifadhiwa kama mafuta mwilini. Hii ni
kwa sababu wana acid ndogo sana tumboni, ndio maana Blood Group A wengi
wanasadikiwa kua na hatari kubwa ya kupata saratani.
Lakini endapo utakula kulingana na kundi lako la damu
lilivyo. Utapata faida nyingi sana. Faida utakazopata kama ukila kulingana na
kundi lako la damu ni kama ifuatavyo;
- 1.
Utaondokana
na maambukizi ya kawaida ya virusi au bacteria.
- 2. Utapungua
uzito (utakua na uzito sahihi) kwa sababu mwili utaondoa sumu (toxins) na
mafuta yaliyojilundika mwilini.
- 3.
Utaweza
kupambana na magonjwa yanayo hatarisha maisha kama vile magonjwa ya moyo,
kisukari pamoja na magonjwa ya ini.
- 4.
Utaepukana
na visababishi vya kuharibu cell za mwili. Hivyo kasi yako ya kuzeeka itapungua
sana.
Vyakula kulingana na kundi lako la damu vimegawanyika katika
sehemu kuu tatu (3);
- 1.
VYENYE MANUFAA SANA = hivi ni vyakula ambavyo ni dawa
kwako
- 2.
VYA UPANDE WOWOTE (NEUTRAL) = hivi ni vyakula ambavyo ni chakula
tu, havina madhara wala faida kubwa.
- 3.
VYA KUEPUKA = hivi ni vyakula ambavyo kwako ni
sumu.
BLOOD GROUP O (THE
HUNTER)
Hili ndio kundi kongwe Zaidi kutokea duniani. Inakadiriwa kua
Group O walikuepo tangu miaka ya 50,000 BC. Hawa wanaitwa wala nyama au
wawindaji. (the hunters).
Hawa wana mfumo wa chakula ambao ni mgumu kiasi na wanafanya
vizuri sana kama wakila protini za juu kama vile nyama. Na hua wanatakiwa
kufanya mazoezi makali, na hii hua inawasaidia kukabiliana na stress.
Group O wana kiwango kikubwa sana cha acid mwilini, na ndio
maana wanahitaji protini nyingi. Lakini pia ndio sababu kwa nini wengi wao
husumbuliwa na vidonda vya tumbo.
VIFUATAVYO NI VYAKULA
AMBAVYO VINAFANYA BLOOD GROUP O WANENEPE;
- 1.
Gluteni ya ngano; hii inaingiliana na uzalishwaji wa
insulin mwilini na hivyo kufanya mfumo wa kimetaboliki (metabolism) kua hafifu.
- 2.
Mahindi ya nafaka (sweetcorn); hii huingilia uzalishwaji wa insulin
na hivyo kufanya kimetaboliki kua hafifu. (Ni mahindi ambayo huvunwa kabla ya
kukomaa vizuri, na yanakua kama yana sukari au matamu).
- 3.
Maharagwe ya figo (kidney bean),
maharagwe ya navy na lenti (lori); haya hufanya utumiwaji wa kalori mwilini kua hafifu.
- 4.
Kabeji, Brussel, koulifulawa
(cauliflower), majani ya haradali; hizi huzuia uzalishwaji wa hormone ya thyroid.
VIFUATAVYO NI VYAKULA
AMBAVYO HUSAIDIA BLOOD GROUP O WAWEZE KUPUNGUA UZITO;
- ·
Kelp (aina ya algae inayoota
pembezoni mwa bahari), vyakula vya baharini, chumvi yenye iodine; hivi vina iodine ambayo inaongeza uzalishwaji
wa hormone ya thyroid mwilini.
- ·
Maini; yana vitamin B ambayo yanasaidia
ufanisi wa kimetaboliki.
- ·
Nyama nyekundu, mboga ya kale,
spinachi, broccoli;
hizi husaidia ufanisi wa kimetaboliki.
JINSI YA KULA KWA BLOOD
GROUP O.
- ·
NYAMA ZENYE MANUFAA SANA; nyama ya ng‘ombe, moyo, figo, nyama
ya kondoo, maini, utumbo (taulo), mkia, swala.
- ·
NYAMA ZA KUEPUKA; nguruwe, goose (bata Bukini)
- ·
VYAKULA VYA BAHARINI VYENYE MANUFAA; blue fish, cod fish (samaki chewa),
sword fish.
- ·
VYAKULA VYA BAHARINI VYA KUEPUKA; baraccuda, cat fish, pweza, smoked
salmon (samaki saroni), cavier, conch (samaki kondomu).
- ·
VYAKULA VITOKANAVYO NA MAZIWA; Group O wanatakiwa kujitahidi
kutokutumia vyakula hivi. Ila wanaweza kutumia soya kama mbadala
- ·
VYAKULA VITOKANAVYO NA MAZIWA VYA
KUEPUKA; jibini
(cheese), maziwa ya mbuzi, ice-cream, skimmed milk, mgando (frozen yogurt)
- ·
Group
O wanafanya vizuri kwenye oils na fats
- ·
MAFUTA YENYE MANUFAA ZAIDI; mafuta ya zeituni (olive oil),
flaxseed oil.
- ·
MAFUTA YA KUEPUKA; mafuta ya nafaka (corn oil), mafuta
ya mbegu za pamba, mafuta ya njugu, mafuta ya alizeti.
- ·
MBEGU ZENYE MANUFAA ZAIDI; mbegu za maboga, walnuts (jozi)
- ·
MBEGU ZA KUEPUKA; korosho, karanga, siagi ya karanga.
- ·
MAHARAGE YENYE MANUFAA ZAIDI; aduki beans (yapo asia kwa sana),
black eyed beans.
- ·
MAHARAGWE YA KUEPUKA; maharagwe ya figo, maharagwe ya
navy, lenti, maharagwe ya soya.
- ·
MBOGA ZENYE MANUFAA; broccoli, kitunguu swaumu, kale,
vitunguu maji, viazi vitamu, pasrley (mboga za pasile), pilipili, maboga
spinachi.
- ·
MBOGA ZA KUEPUKA; parachichi, kabichi, koulifulawa,
uyoga, viazi, zeituni, sweetcorn.
- ·
MATUNDA YA KUEPUKA; nazi, blackberries, tikiti,
machungwa, strawberries, plantains (ndizi za kupika)
- ·
VINYWAJI VYA KUEPUKA; kahawa, soda
BLOOD GROUP A (THE
CULTIVATORS)
• Hawafanyi vizuri wakila protini za
nyama. (zinaongeza mucus {belaghami} kwenye mfumo wao wa hewa) ila wanafanya
vizuri sana kwenye protini za mimea kama soya na tofu
• Ndio wa kwanza kutumia mbogamboga
• Mfumo wao wa chakula upo sensitive
sana
• Wanadili na stress kwa vitendo vya
utulivu kama yoga.
• Wana hatari kubwa ya magonjwa ya
moyo, saratani na kisukari ki biologia.
• Wanahifadhi nyama mwilini kama mafuta
• Wana acid ndogo sana tumboni
• Vyakula vitokanavyo na maziwa sio
vizuri sana kwao
VYAKULA VINAVYOPELEKEA GROUP A KUONGEZEKA UZITO.
• Nyama; haimeng‘enywi vizuri na
inahifadhiwa kama mafuta.
• Vyakula vya maziwa; vinachochea reaction ya insulin na
hupelekea kimetaboliki kua hafifu.
• Maharagwe ya lima; yanafanya kimetaboliki kua hafifu.
• Ngano(ya kias kikubwa); inafanya misuli kua na acid, hivyo
kufanya uhafifu wa matumizi ya kalori.
VYAKULA VINAVYOPELEKEA
GROUP A KUPUNGUA UZITO.
• Mafuta ya mboga (vegetable oil); yanawezesha mmeng‘enyo mzuri,
yanasaidia kuzuia maji mengi kubaki mwilini. (fluid retention)
• Vyakula vya soya; vinawezesha mmeng‘enyo mzuri wa
chakula, kimetaboliki kua na ufanisi, vinaweka sawa kinga ya mwili.
• Mbogamboga; zinafanya ufanisi mzuri wa
kimetaboliki.
• Nanasi; inaongeza ufanisi wa tumbo,
inaongeza ufanisi wa utumiaji wa kalori.
• Group A wanafanya vizuri kama
wasipotumia nyama, ila wanaweza kutumia samaki badala ya nyama.
ULAJI WA VYAKULA KWA GROUP A.
• NYAMA ZA KUEPUKA; nguruwe, kondoo, maini, nyama ya
ng‘ombe, bata, moyo, figo.
• VYAKULA VYA BAHARINI; ni vizuri sana kwa Group A
• VYAKULA VYA BAHARINI VYA KUEPUKA; barracuda, bluefish, catfish, kaa,
lobster (Kambamti), pweza, ngisi.
• VYAKULA VYA MAZIWA; hawapaswi kutumia chochote
kilichotengenezwa na whole milk au mayai. Ila wanaweza kutumia maziwa ya soya
na jibini ya soya kama mbadala.
• VYAKULA VYA MAZIWA VYA KUEPUKA; jibini, siagi, ice-cream, maziwa.
• OIL & FAT ZENYE MANUFAA; mafuta ya flaxseed (kitani), mafuta
ya zeituni
• MAFUTA YA KUEPUKA; corn oil (mafuta ya nafaka), mafuta
ya mbegu za pamba, mafuta wa njugu, mafuta ya sesame (ufuta)
• MBEGU ZENYE MANUFAA; karanga(nzuri kwa kupigana na seili
za saratani), siagi ya karanga, mbegu za maboga.
• MBEGU ZA KUEPUKA; korosho.
• MAHARAGWE YENYE MANUFAA; maharagwe ya adzuki, maharagwe
meusi, maharagwe mekundu ya soya
• MAHARAGWE YA KUEPUKA; kidney beans, maharagwe ya lima,
maharagwe ya Navy, maharagwe mekundu.
• VYAKULA VYA NAFAKA VYENYE MANUFAA; buckwheat (ngano isiyo na gluten),
amaranth, unga wa mchele, unga wa oat,
• NAFAKA ZA KUEPUKA; cream ya ngano, wheat bran, unga wa
ngano (whole wheat flour)
• MBOGAMBOGA ZENYE MANUFAA; broccoli, kitunguu swaumu, kale,
kitunguu maji, tofu, maboga, spinachi.
• MBOGAMBOGA ZA KUEPUKA; kabichi, pilipili ya chili, uyoga,
zeituni, viazi, nyanya, magimbi.
• MATUNDA YENYE MANUFAA; grapefruit, limao/ndimu, nanasi
• MATUNDA YA KUEPUKA; ndizi mbivu, nazi, machungwa, ndizi
za kupika, maembe, tikiti, papai.
• VINYWAJI VYENYE MANUFAA; mvinyo mwekundu (red wine) ni nzuri
kwa afya ya moyo, kahawa, green tea.
• VINYWAJI VYA KUEPUKA; bia, spirit, chai, soda.
BLOOD GROUP B (THE NOMAD)
• wapo na balance (kama jina lao)
• Wana kinga yenye nguvu
• Wanauwezo wa kula vitu vingi tofauti
Zaidi, walaji wa vyakula vitokanavyo na maziwa.
• Wanadili na stress kwa kufanya
shughuli za ubunifu.
• Wanauwezo wa kushinda magonjwa mengi
makubwa kama magonjwa ya moyo na saratani
• Ni rahisi kupata matatizo yanayotokana
na udhaifu wa kinga ya mwili kama vile chronic fatique syndrome (ugonjwa wa
kuchoka sana), multiple sclerosis (ugonjwa unaokula nerves), lupus (kinga ya
mwili inakula tissue zake zenyewe)
VYAKULA VINAVYOWAONGEZEA UZITO GROUP B
• Sweetcorn; inazuia uzalishwaji wa insulin,
inaingilia ufanisi wa kimetaboliki.
• Lenti; inasababisha sukari kushuka,
inazuia virutubisho kufika mwilini vizuri, inaingilia ufanisi wa kimetaboliki
• Karanga; inaingilia ufanisi wa kimetaboliki,
inashusha sukari, inazuia ufanisi wa kazi wa ini
• Mbegu za ufuta; zinaingilia ufanisi wa
kimetaboliki, zinasababisha kushuka kwa sukari.
• Ngano; inazuia ufanisi wa kimetaboliki,
inashusha sukari, inasababisha chakula kutunzwa kama mafuta badala ya energy
(nguvu)
VYAKULA VINAVYOWAPUNGUZIA UZITO GROUP B
Mboga za majani, nyama, maini, mayai; yanasaida ufanisi wa kimetaboliki
ULAJI WA CHAKULA KWA GROUP B
• VYAKULA VYA NYAMA VYENYE UMUHIMU; kondoo, sungura
• VYAKULA VYA NYAMA VYA KUEPUKA; nguruwe, kuku, moyo, bata, quail,
patridge.
• VYAKULA VYA BAHARINI; ni vizuri kwa type B
• VYAKULA VYA BAHARINI VYA KUEPUKA; barracuda, kaa, crayfish, lobster,
pweza, Kamba (prawns), smoked salmon.
• VYAKULA VITOKANAVYO NA MAZIWA VYENYE
UMUHIMU; jibini,
maziwa ya mbuzi, skimmed milk, mtindi
• VYA KUEPUKA; ice-cream.
• OIL & FAT YENYE MANUFAA; mafuta ya zeituni.
• MAFUTA YA KUEPUKA; corn oil, mafuta ya mbegu za pamba,
mafuta ya njugu, mafuta ya alizeti, ufuta.
• MBEGU; mara nyingi sio nzuri kwa B, ila
waepuke korosho, karanga na siagi yake, ufuta, alizeti
• MAHARAGWE YENYE MANUFAA; maharagwe ya figo, maharagwe ya
lima, navy beans.
• MAHARAGWE YA KUEPUKA; adzuki beans, maharagwe meusi.
• NAFAKA ZENYE MANUFAA; mtama, oat bran, mchele.
• NAFAKA ZA KUEPUKA; ngano, cornflakes, corn meal.
• MBOGAMBOGA ZENYE MANUFAA; Brussel, kabichi, karoti, koulifulawa,
kale, uyoga, haradali, parsley, pilipili, viazi vitamu, magimbi.
• MBOGAMBOGA ZA KUEPUKA; parachichi, zeituni, boga,
sweetcorn, tofu, nyanya.
• MATUNDA YENYE MANUFAA; ndizi mbivu, cranberries, zabibu,
papai, nanasi.
• MATUNDA YA KUEPUKA; nazi, komamanga, starfruit,
prickley pears.
• VIUNGO; waepuke kutumia mdalasini.
• VINYWAJI VYENYE MANUFAA; green tea
• VINYWAJI VYA KUEPUKA; spirits, soda
BLOOD GROUP AB (The Enigma)
•
Mchanganyiko wa A na B
•
Tabia kama za kinyonga, kwenye kukabiliana na
mazingira au milo yao
•
Wana mfumo wa kula ambao ni sensitive.
•
Kinga yao ipo kimya sana.
•
Wanadili na stress kwa kiroho Zaidi, mazoezi na
ubunifu
•
Wana risk kubwa ya saratani kwa sababu wana
mchanganyiko wa A na B, hivyo mbaya wa B na mbaya wa A, kwa AB anaweza kua
rafiki.
•
Kinga yao haijatulia (compex), hii ni sifa
inayowapa wengine Nguvu na wengine udhaifu.
VYAKULA
VINAVYOWAONGEZEA UZITO GROUP AB
•
Nyama nyekundu; mmeng‘enyo wake ni wa tabu na inahifadhiwa kama mafuta.
•
Kidney beans, lima beans, mbegu, sweetcorn
(nafaka au mahindi yaliovunwa kabla ya kukomaa), ngano; zinazuia kuzalishwa kwa insulin hivyo kushuka kwa sukari
•
Ngano;
inashusha ufanisi wa kimetaboliki na utumiwaji wa kalori.
VYAKULA VYA
KUPUNGUZA UZITO KWA GROUP AB
•
Tofu, vyakula vya baharini, mboga za majani; zinasaidia ufanisi wa kimetaboliki.
•
Kelp, vyakula vya maziwa; vinaongeza ufanisi wa kuzalishwa kwa
insulin.
•
Matunda ya alkaline (zabibu, nanasi, tikiti
maji,apple n.k); yanaongeza
alkaline kwenye misuli.
•
Nanasi;
linasaidia mmeng‘enyo wa chakula, inaongeza ufanisi wa ufanyaji kazi wa tumbo.
ULAJI WA VYAKULA
WA GROUP AB
•
NYAMA ZENYE MANUFAA; kondoo, sungura, turkey (Bata Mzinga).
•
NYAMA ZA KUEPUKA; nyama ya ng‘ombe, nyama ya nyati, kuku, bata, nguruwe, moyo,
quail.
•
VYAKULA VYA BAHARINI VYENYE MANUFAA; tuna, cod, mackerel, red fish,
grouper, mahi mahi.
•
VYAKULA VYA BAHARINI VYA KUEPUKA; barracuda, kaa, crayfish, lobster,
pweza, chaza (oysters), smoked salmon (samaki saroni).
•
VYAKULA VYA MAZIWA; mayai ni mazuri kwa AB, jibini ya cottage, jibini ya farmers,
•
VYAKULA VYA MAZIWA VYA KUEPUKA, jibini ya bluu, brie, siagi, maziwa
ya siagi, ice-cream,
•
MAFUTA YENYE MANUFAA; mafuta ya zeituni
•
MAFUTA YA KUEPUKA; corn oil (mafuta ya nafaka), mafuta ya mbegu za pamba, mafuta ya
alizeti, mafuta ya ufuta.
•
MBEGU ZENYE MANUFAA; chestnuts, karanga na siagi yake, walnuts
•
MBEGU ZA KUEPUKA; hazelnuts, mbegu za poppy, mbegu za maboga, mbegu za ufuta, mbegu
za alizeti.
•
MAHARAGWE YENYE MANUFAA; lenti, navy beans, maharagwe ya
pinto, maharagwe mekundu, maharagwe ya soya.
•
MAHARAGWE YASIYOFAA; adzuki, maharagwe meusi, maharagwe ya figo, maharagwe ya lima.
•
NAFAKA ZINZOFAA; mtama, oat bran, rice bran, mchele, *kwa wenye pumu (asthma)
wanatakiwa wasitumie ngano kwa sababu inachochea kuzalishwa kwa mucus kwenye
mfumo wa hewa, unga wa oat, unga wa mchele
•
NAFAKA ZA KUEPUKA; ngano, cornflakes, cornmeal
•
MBOGAMBOGA ZENYE MANUFAA; alfalfa, broccoli, koulifulawa,
tango, kitunguu swaumu, kale, uyoga, haradali, parley, tofu, magimbi.
•
MBOGAMBOGA ZA KUEPUKA; parachichi, pilipili ya chili, zeituni, sweetcorn.
•
MATUNDA YENYE MANUFAA; cherries, mtini (fig), zabibu,
•
MATUNDA YA KUEPUKA; ndizi, nazi, pera, maembe, komamanga, prickly pears, starfruit.
•
VIUNGO VYENYE MANUFAA; curry powder,
parley,
•
VIUNGO VYA KUEPUKA; almond (mlozi)
cornflour, corn syrup, pilipili.
•
VINYWAJI VYENYE MANUFAA; kahawa, green
tea
•
VINYWAJI VYA KUEPUKA; spirit,
chainyeusi,soda
Tukumbuke kua, vyakula vyenye manufaa
ni vile ambavyo ni kama dawa, vyakula vya upande wowote (neutral) ni ambavyo ni
vyakula tu, na vyakula vya kuepuka ni ambavyo ni kama sumu. Hivyo kama kuna
vyakula sijavitaja, ujue hivyo ni neutral, na unaweza tu kutumia kama kawaida.
Lakini vya kuepuka ujue kwako vina madhara Zaidi kuliko faida.
Pia najua unaweza usiifwate nadharia
hii kwa 100%, lakini unaweza kujitahidi kwa kiasi flani, haswa haswa kama
unasumbuliwa na magonjwa mbali mbali au kama unapata changamoto katika kupungua
uzito.
FOOD IS MEDICINE, chakula sahihi ndio dawa ya kwanza kabla ya dawa nyingine yoyote ile,
ndio maana watu ambao wanakula mlo sahihi, hua hawasumbuliwi na magonjwa, kua
na uzito mkubwa na hua miili yao ina nguvu sana kulinganisha na weingine.
kwa msaada Zaidi juu ya nadharia
(theory hii) unaweza kusoma kitabu kinachoitwa EAT RIGHT FOR YOUR BLOOD TYPE kilichoandikwa na Dr
Peter D’Adamo 1996
Nadharia hii haijathibitishwa kabisa
kitaalam, ingawa baadhi ya tafiti zinasema kua watu wengi imewasaidia
Hivyo unaweza kuitumia au usiitumie,
cha msingi ni kuzingatia ulaji sahihi na kuepuka ulaji mbovu kwa ajili ya afya
zetu.
Imeandikwa na SAMUEL MACHA
FIT BY WAYNE.
CONTACTS:
Mobile: 0753068572
Whatsapp: 0621068072 WHATSAPP
Comments
Post a Comment