Skip to main content

FANYA HIVI KUIMARISHA NGUVU ZA KIUME

 

NJIA ZA ASILI ZA KUTATUA UKOSEFU WA NGUVU ZA KIUME.

Hapo zamani, ilizoeleka wazee tu ndio wanakua na shida kwenye nguvu za kiume, na ni kwa sababu ya magonjwa ya moyo, kisukari pamoja na kuzeeka ambapo hufanya mwili kudhoofika na kushindwa kwa baadhi ya mambo.

lakini siku za hivi karibuni, hata vijana wadogo kabisa ambao hawajafika miaka 30 huathiriwa na ukosefu wa nguvu za kiume, na hii ni kutokana na sababu mbalimbali, ulaji mbovu na mtindo wa maisha vikiwa vinachangia kwa kiasi kikubwa.

VISABABISHI VYA UKOSEFU WA NGUVU ZA KIUME.

  • Upigaji wa Punyeto kwa muda mrefu: vijana wengi hutumia mikono yao ambayo kwa kawaida ina ngozi ngumu kuliko uke wa mwanamke, hivyo hufanya mishipa ya uume kulegea, pia kisaikolojia huwezi kupiga punyeto bila kuvuta picha ya mwanamke flani kichwani.
  • Magonjwa ya moyo
  • Uzito Uliozidi (Obesity)
  • Kisukari
  • Uvutaji wa sigara na dawa za kulevya
  • Shinikizo la juu la damu (High blood pressure)
  • Utumiaji wa pombe kupita kiasi
  • Sonona na msongo wa mawazo
  • Kuumia/ kupata ajali inayoathiri maeneo ya uzazi
  • Upungufu wa homoni ya testosterone
  • na sababu nyinginezo

NJIA ZA KUTATUA CHANGAMOTO YA NGUVU ZA KIUME

  • Shughulisha mwili kwa kufanya mazoezi: itakusaidia kua na stamina, mzunguko wa damu kua vizuri hadi kwenye mishipa midogo midogo.
  • Zingatia mlo mzuri
  • Jitahidi kuepukana na msongo wa mawazo
  • Epuka kutumia sigara na pombe kabisa.
  • pata msaada zaidi kwa daktari inapobidi.

FWATA MFUMO HUU WA KULA ILI KUIMARIKA.

  • kila asubuhi, jitahidi kunywa chai yenye tangawizi (ikiwezekana usiweke sukari) pamoja na muhogo, gimbi au viazi vitamu. (ila usitumie vya kukaanga)
  • mchana unaweza kutumia Ugali wa Dona au wa Mtama (wa sembe sio mzuri sana), na usikose kutumia mboga za majani. (ila usitumie chainizi). kama inawezekana, mboga iwe imeungwa kwa karanga au nazi (ikiwa inawezekana). Shushia na ndizi mbivu kama tunda au tikiti maji (tafuna na zile mbegu zake, ninashangaa sana mwanaume unapokula tikiti na kutema zile mbegu)
  • Jioni kula chakula chako chochote (jitahidi usitumie vyakula vilivyokobolewa) pamoja na ndizi mbivu kama tunda lako au tikiti maji na utafune na mbegu zake.
  • kila siku mchana unaweza ukatafuna karanga kama utazipata, na glass ya mtindi muda ambao unakua umetulia. (mtindi usitumie ule uliowekwa sukari.)
Ikiwa Utapenda kupata Dawa ya Asili kwa ajili ya changamoto ya Nguvu za kiume, tafadhali bonyeza HAPA

Imeandikwa na:
SAMUEL MACHA
FIT BY WAYNE


Contacts:
mobile: 0753068572
whatsapp: WHATSAPP

















Comments

Popular posts from this blog

DETOX YA SIKU 7. HATUA YA KWANZA KUPUNGUZA UNENE

  HATUA YA KWANZA KUPUNGUZA UNENE. Uzito Unaotakiwa kua nao Kulingana na Urefu Pamoja na Jinsia UREFU (CM) UREFU (FT & INCH) UZITO (KG)       MWANAUME MWANAMKE 147 4' 10" - 45-59 150 4' 11" - 45-60 152 5' 0" - 46-62 155 5' 1" 55-66 47-63 157 5' 2" 56-67 49-65 160 5' 3" 57-68 50-67 162 5' 4" 58-70 51-69 165 5' 5" 59-72 53-70 167 5' 6" 60-74 54-72 170 5' 7" 61-75 55-74 172 5' 8" 62-77 ...

BAWASIRI NA JINSI YA KUITIBU KWA NJIA ZA ASILI

 BAWASIRI NA JINSI YA KUITIBU KWA NJIA ZA ASILI.   💊💊💊💊💊💊💊💊💊💊💊💊💊   BAWASIRI NI NINI?   Bawasiri (kikundu, future, puru au mjiko ) ni hali ya kutuna kwa mishipa ya damu katika mfereji wa sehemu ya haja kubwa (anus). Kuna aina mbili za Bawasiri;   1. Bawasiri za ndani ( internal haemorroids )   2. Bawasiri za nje ( external haemorroids )  Bawasiri za ndani hua na dalili ya kupata kinyesi kilichokua na damu,  bawasiri za nje hua na dalili ya maumivu makali wakati wa kujisaidia pamoja na kinyama kutoka kwa nje.  NINI VISABABISHI VYA BAWASIRI?   1️⃣Historia ya familia, mara nyingi baadhi ya familia hukumbwa na changamoto hii. Na hua watu wa familia hiyo husika wanakua na hili tatizo. 2️⃣Kupata choo kigumu mara kwa mara husababisha mtu kutumia nguvu nyingi (straining) ambayo husababisha bawasiri kutokea. 3️⃣Unene (uzito uliopitiliza) hua ni kisababishi cha bawasiri kwa sababu ya kuongezeka kwa Rectal Vein Pressure. 4️⃣Ku...

CALORIE ZA VYAKULA VYA TANZANIA

 CALORIES ZA VYAKULA TANZANIA   NINI MAANA YA CALORIE?    Calorie ni kiasi cha nishati kinachohitajika ili kuongeza joto la gramu moja ya maji (°C). Kwa lugha nyepesi, calorie katika chakula hutoa nishati (energy) kwa njia ya joto ili miili yetu iweze kufanya kazi. Hii ni kwa sababu miili yetu huhifadhi na kuchoma calorie kama mafuta.  UHUSIANO WA CALORIE NA UZITO WA MWILI.  Kwa kawaida, kila chakula kina kiwango chake cha calorie. Hivyo unapokula chakula, unaingiza mwilini calorie kadhaa, na mwili wako pia unatumia calorie katika kuweka uhai. Lakini unapokula chakula, unaingiza calorie mwilini. Na mwili wako pia unatumia calorie kama nishati. Hivyo unapokula calorie nyingi kuliko mwili unavyoweza kutumia, zinahifadhiwa kama mafuta na utaongezeka uzito. Unapotumia calorie nyingi kuliko unavyoingiza mwilini, unapungua uzito. Na ukitumia kiasi sawa na unachoingiza, basi unabaki na uzito ule ule.   MWANADAMU ANAHITAJI WASTANI WA CALORIE NGAPI? ...