Skip to main content

Posts

Showing posts from January, 2022

Vyakula 8 Vinavyosaidia Kusafisha Damu Kwa Asili

  Vyakula 8 Vinavyosaidia Kusafisha Damu Kwa Asili. Mara zote huwa tunavuta hewa, tunakula pamoja na kunywa kemikali za hatari na kuingiza katika miili yetu. Miili yetu hua inafanana sana na injini mfano magari. Gari ni lazima ulifanyie service kama vile kubadilisha oil n.k kila baada ya muda flani. Vivyo hivyo na miili yetu, ni lazima kujifunza kuisafisha na kuondoa taka mwili ambazo huingia kupitia njia mbali mbali kila siku. Katika mlo wako wa kila siku, kuna vyakula unaweza kuviongeza na vikasaidia sana kusafisha mwili wako kuanzia ndani. 1. Giligilani Majani ya giligilani Zina wingi wa vitakasa sumu ( antioxidants ) pamoja na Vitamin A, K pamoja na C, husaidia moyo, Figo pamoja na Ini kuondoa taka mwili ambazo hujishikiza humo. Mafuta yaliyomo kwenye giligilani ( volatile Oil ) husawazisha seli zinazosababisha saratani. Juisi ya giligilani husaidia sana afya ya macho pamoja na kuzuia uono hafifu wa macho kwa kuongeza mtiririko wa damu kwenye mishipa midogo midogo kwenye macho. Tum

MADHARA 6 MAKUBWA YATOKANAYO NA KUNYWA SODA.

  MADHARA 6 MAKUBWA YATOKANAYO NA KUNYWA SODA. Soda hua ni kinywaji chenye sukari nyingi sana na kisicho na faida yoyote mwilini. (No nutritional value) ingawa watu wengi hupendelea kutumia katika nyakati tofauti. Soda ni kinywaji chenye madhara mengi sana mwilini kuliko faida, na ni kinywaji ambacho ni vyema kukiepuka, ingawa watu wengi hupendelea hata kuwapa watoto watumie bila kujua ya kwamba wanahatarisha maisha yao ya sasa na baadae. MADHARA YATOKANAYO NA KUNYWA SODA. Ugonjwa wa Kimetabiliki (metabilic Syndrome) : Matumizi ya Soda moja kwa siku huongeza hatari ya kupata ugonjwa wa kisukari kwa asilimia 67% Afya ya Ngozi kudhoofika : Soda hua na kemikali inayoitwa Flame-Retardant Brominated Vegetable Oil (BVO ), ni kemikali inayodhoofisha afya ya ngozi pamoja na mfumo wa neva za fahamu.  Huongeza Kasi ya Uzee : Soda ina Phosphate pamoja na Phosphoric acid ambazo hutumika kufanya soda zikae muda mrefu bila kuharibika. Ila husababisha kuongezeka kwa kasi ya uzee na kusinyaa kwa ngo

MKAKATI WA KUIMARISHA AFYA YAKO MWAKA 2022

  UNA MKAKATI GANI ILI KUIMARISHA AFYA YAKO? kuna msemo hua napenda sana kuutumia, ya kwamba  MJI WA ROMA HAUKUJENGWA KWA SIKU MOJA. Hii inamaanisha ya kwamba, afya ya mtu ilivyo, ni matokeo ya alivyozoea kula kwa kipindi cha muda flani. Hamna mtu aliyenenepa kwa siku moja, wala aliyepungua kwa siku moja. ila vyote huhusisha mazoea ya namna flani ambayo ndio husababisha mtu kua na afya ya namna flani. Mara nyingi watu hupenda sana kupungua ndani ya muda mfupi, tena bila kuweka juhudi katika kupungua, lakini wanasahau ya kwamba, hata unene walionao haukuja kwa muda mfupi. Bali umechukua muda flani wao kufikia unene huo waliokua nao. Ili uweze kua na uzito sahihi (uzito sahihi hukufanya kuepukana na magonjwa mengi yasioambukizwa ambayo ni hatarishi), Ni lazima uanze kufanya baadhi ya vitu. lakini sio kufanya tu, inabidi viwe tabia yako ya kila siku. Na endapo vitu hivyo vikiwa tabia, basi ndani ya muda flani Afya yako itaimarika zaidi na zaidi. TABIA 10 AMBAZO ZITAKUWEZESHA KUA NA UZITO