VIRUTUBISHO 6 VYENYE AFYA Virutubisho ni dutu (substance) ambazo hurutubisha mwili na afya kwa ujumla. Virutubisho hupatikana kwenye vyakula tunavyokula au kunywa kila siku. Japokua, kila tunachokula au kunywa, hytofautiana virutubisho vinavyopatikana. Kuna ambavyo vimejaa virutubisho, na kuna ambavyo havina virutubisho na hivyo kua havina faida kwenye mwili wa mwanadamu ingawa vinaonekana kua na ladha nzuri. VIRUTUBISHO 6 VYENYE AFYA NA VYAKULA VYAKE. 1. NYUZI NYUZI Nyuzi nyuzi husaidia sana kuratibu uzito wa mwili, kupunguza hatari za kisukari na lehemu (cholesterol) kwenye damu, Pia kupunguza athari za magonjwa ya moyo. Nyuzi zisizo yeyuka husaidia sana kuweka mfumo wa chakula na msukumo uende kwa urahisi. vyakula Vyenye nyuzi nyuzi ni kama vile Njegere, karoti, maharage mabichi, cauliflower, viazi vitamu, matunda 2. VITAMIN A Husaidia sana kuona kwa macho na kukinga mwili dhidi ya magonjwa ya kuambukiza. Pia husaidia kuwezesha nyama za mifupa, ngozi na meno kuwa na afya nzuri.
Blog hii ni kwa ajili ya kukusaidia kutatua changamoto za ki afya ambazo zinaweza kutatulika kwa kubadilisha jinsi ya kula na mtindo wa maisha