Skip to main content

Posts

Showing posts from February, 2021

WASTANI WA KUPUNGUA UZITO KWA MWEZI.

  wastani wa kupungua WASTANI WA KUPUNGUA KWA MWEZI.  Bila shaka kama una uzito mkubwa, umeshawahi kutamani ungepunguza kilo nyingi sana ndani ya muda mfupi. Lakini je, unatakiwa kupungua wastani wa kilo ngapi kwa mwezi? Pia umeshawahi kuona ya kwamba kuna mtu anapungua haraka sana ndani ya muda mfupi, lakini baada ya muda mfupi ananenepa tena, na pengine Zaidi ya mwanzo. Na vile vile kuna ambae anapungua kwa mwendo wa kawaida, lakini akishapungua na kufikia uzito sahihi, basi hanenepi tena. Au hanenepi kwa urahisi.  JE, NI WASTANI WA KILO NGAPI UNATAKIWA KUPUNGUA KWA MWEZI?  Wataalam wa afya wanashauri ya kwamba upungue uzito kwa spidi ambayo ni ya wastani au kawaida, yaani sio ya haraka sana kupita kiasi. Hii itakusaidia kua na uzito sahihi kwa muda mrefu Zaidi. Kupungua uzito hutegemea UMRI , JINSIA , UCHANGAMFU WA MTU (PHYSICAL ACTIVITY LEVEL/MAZOEZI) pamoja na MATOKEO YA DAWA/DOZI MBALI MBALI . Hivyo kila mtu huenda kwa spidi yake. Kwa kawaida, ni afya Zaidi kupungua kuanzia kilo

USITUMIE VYAKULA HIVI KAMA UNA UMRI WA MIAKA 30 AU ZAIDI

  USILE VYAKULA HIVI KAMA UNA UMRI WA MIAKA 30 AU ZAIDI  'The doctors of the future will no longer treat the human frame with drugs, but rather will cure and prevent disease with nutrition’ - Thomas Edison.  Lishe ndio kitu kikubwa Zaidi katika kuboresha au kubomoa afya ya mwanadamu. Na kwa kutumia lishe pekee, una uwezo wa kufanya mwili wako uwe na uwezo mkubwa wa kujitibu wenyewe. Kama una umri (au utakapofikisha umri) wa miaka 30 na Zaidi, basi vyakula hivi jitahidi kuviepuka.    Pombe : hua ina kalori nyingi sana, na kuanzia umri wa miaka 30 mwili hauwezi tena kuzichoma zote na hivyo kuhifadhiwa kama mafuta na kusababisha kitambi/unene. Pia inabadilisha kiwango cha insulini na kusababisha kua na hamu ya kula vitu vyenye sukari.   Sukari za kutengenezwa: hizi husababisha mwili wako usitumie kalori zake vizuri na pia huongeza hatari ya saratani. Pia husababisha glucose kuwepo kwa kiwango kikubwa na kupunguza ufanisi wa insulini. Hivyo kusababisha kuongezeka kwa uzito, magonjwa

MLO SAHIHI KULINGANA NA KUNDI LA DAMU (BLOOD GROUP)

  MLO SAHIHI KULINGANA NA KUNDI LAKO LA DAMU (BLOOD GROUP) Kuna msemo unaosema kua ONE MAN ' S FOOD IS ANOTHER MAN ' S POISON . Yaani ikiwa inamaanisha kua. Chakula ambacho kina manufaa kwako, huenda kikawa ni sumu kwa mtu mwingine. Sasa najua utajiuliza kua kwa nini ipo hivi. Hii ni kwa sababu sisi tupo vile tulivyo kulingana na kundi la damu tulilo nalo. Damu ni uhai, damu haielezeki kiurahisi. Lakini ndio inatupa uhai sisi binadamu na viumbe vingine vyote. Lakini je, kutokana na makundi ya damu tuliyonayo, ni sahihi kila kundi kula mlo mmoja?? Labda nitoe mfano kidogo; Blood group O wanafanya vizuri sana wakila protini kama nyama, kwa sababu hawa hua wana acid nyingi tumboni, na ndio maana Blood Group O wengi wana vidonda vya tumbo. Lakini blood group A wanafanya vizuri sana kama wakila mboga za majani. Kwa sababu wakila nyama inawatesa kwenye mmeng ' enyo wa chakula na huhifadhiwa kama mafuta mwilini. Hii ni kwa sababu wana acid ndogo sana tumboni, ndio maana Bloo