JINSI MWANAMKE ANAVYOWEZA KUZUIA AU KUKABILIANA NA VIMBE KWENYE KIZAZI (FIBROIDS). Fibroids ama vimbe kwenye kizazi ni tatizo la kihomoni ambalo linatokea kwa mwanamke ambae yupo katika umri wake anaoweza kuzaa. Hii humaanisha ya kwamba fibroids hua zinalishwa na homoni ya oestrogen. Fibroids ni kama magugu ambayo huota shambani katika shamba ambalo halifanyiwi palizi au limeachwa. Wanawake walio katika hatari ya kupata fibroids ni;- · Wanawake wenye umri kuanzia miaka 28, japokua hata chini ya miaka 28 wanaweza kupata. · Wanawake wanene. · Wanawake weusi (waafrika); hii ni kwa sababu ya ulaji pamoja na mtindo wa maisha. · Wanawake wenye shida ya presha pamoja na kisukari. · Historia ya familia kua na fibroids. Familia huambukizana epigenetics na endocrine disruptors kutokana na tabia ya ulaji na mtindo wa maisha ya familia husika. · Wanawake ambao hawajazaa. Haswa ambao wamefika miaka 30. · Wanawake wenye upungudu
Blog hii ni kwa ajili ya kukusaidia kutatua changamoto za ki afya ambazo zinaweza kutatulika kwa kubadilisha jinsi ya kula na mtindo wa maisha