JE, MAJI YA MOTO HUSAIDIA KUPUNGUZA KITAMBI? Bila shaka umeshawahi kuona watu ambao hunywa maji ya moto na limao kila asubuhi huku wakisema ya kwamba wanafanya hivyo ili kupunguza kitambi. Cha ajabu ni kwamba watu hawa wanafanya hivi lakini hawafanyi mabadiliko yoyote juu ya vyakula wanavyokula au mtindo wa maisha. Kwa kifupi ni kwamba, ukiona mtu anasema anakunywa maji ya moto kwa lengo la kupunguza kitambi, ujue ni mvivu wa kubadilisha mtindo wake wa maisha na anapenda njia za mkato. Ila ukweli ni kwamba, katika kupunguza unene na kuondokana na kitambi, hua hamna njia za mkato. UKWELI KUHUSU MAJI YA MOTO Maji ya moto hayayeyushi mafuta kama wengi wanavyodhani. Na pia hayana mchango wowote katika kuyeyusha mafuta yanayosababisha unene mwilini mwa mwanadamu. Tindikali ya Hydrocloric tumboni ndio husaidia katika kumeng`enya chakula, lakini sio maji ya moto. Mtu anayekunywa maji ya moto na anayekunywa maji ya baridi, wote wanakunywa maji. Na hamna kitu cha ziada kinachowa
Blog hii ni kwa ajili ya kukusaidia kutatua changamoto za ki afya ambazo zinaweza kutatulika kwa kubadilisha jinsi ya kula na mtindo wa maisha