Skip to main content

Posts

Showing posts from April, 2022

Mbinu za Kukusaidia Kua Mwanaume Rijali na Kuondokana na Upungufu wa Nguvu za Kiume

  Mbinu Zinazosaidia Kua Mwanaume Rijali na Kuondoa Upungufu Wa Nguvu Za Kiume. Upungufu wa nguvu za kiume (Erectile Dysfunction) ni hali ya kukosa uwezo wa kudumisha kusimama kwa uume wakati wa kufanya ngono. Hali hii huleta fedheha ambayo huteteresha mahusiano yaliyo mengi, husababishwa na matukio au hali ambazo huvuruga utimamu wa misuli, vhichochezi (hormones), mishipa ya fahamu pamoja na mishipa ya damu katika uume. Visababishi Vya Upungufu Wa Nguvu Za Kiume. Sababu za Kisaikolojia Sababu za kimetaboliki Sababu za mfumo wa neva za fahamu pamoja na mifupa ya misuli. 1. Sababu za Kisaikolojia Sonona/ msongo wa mawazo Unywaji wa pombe na sigara: (hudhoofisha mfumo wa neva, ubongo pamoja na mishipa ya damu kadiri mtumiaji anavyotumia) Wasiwasi Hali ya hatia Kujiona huna thamani (low self esteem) Picha ama video za ngono na punyeto: Hizi ndio mbaya zaidi kwani huleta ganzi katika sehemu zihusikazo na ladha za kimahaba katika ubongo. 2. Sababu Za Kimetaboliki Ugonjwa wa kisukari Shiniki

Nini Cha Kufanya Endapo Unaugua (Au mtoto kuugua) Mafundofundo Mara Kwa Mara

Mafundofundo Tonsillitis, Tonsils, Mafundofundo, Matezi. Tonsillitis ni inflammation ya Tonsils pale ambapo mwili hushambuliwa na bacteria au virusi. Tonsilitis ni tishu 2 zenye umbo la mviringo zinazopatikana nyuma ya koromeo pande mbili za ulimi. Tonsils ni mstari wa mbele katika kinga ya mwili. Hizi huzuia vimelea hatarishi kabla havijafika katika mfumo wa mwili. Tonsils zinapokamata vimelea, na zenyewe hupata inflammation na kupelekea hali ijulikanayo kama Tonsillitis ambapo huvimba na kua na mamumivu pale unapokua unameza kitu. Mara nyingi watu haswa watoto hupata Tonsillitis na kwenda hospitali kutibiwa kwa antibiotics. Ila kuna ambazo zinajirudia mara kwa mara hata kama zikitibiwa kwa dawa. Mara nying8 katika hali ya kujirudia mara kwa mara, wengi hushauriwa kufanya upasuaji mdogo ujulikanao kama Tonsilectomy ili kuziondoa. Ikiwa Tonsils ndio mstari wa mbele wa kinga, ni kwa nini ziondolewe? Nini Kifanyike Endapo Tonsillitis Inajirudia Mara kwa Mara. Epuka kabisa sukari na vitu