Mazoezi NAMNA YA KUFANYA MAZOEZI KWA AFYA. Mazoezi ni shughuli yoyote ya mwili ambayo huongeza au kudumisha utimamu wa mwili, afya na ustawi kwa ujumla. NI KWA NINI WATU HUFANYA MAZOEZI? kusaidia ukuaji wa mwili kuboresha nguvu ya mwili kupunguza kasi ya uzee kuboresha au kukuza misuli kuboresha mfumo wa moyo na mishipa kuboresha ujuzi wa riadha kupunguza uzito/unene au kudumisha uzito sahihi kuboresha afya starehe na sababu nyinginezo ISTILAHI MUHIMU ZA KUZIJUA Kabla ya kuona jinsi ya kufanya mazoezi kadhaa, ni vyema kufahamu istilahi chache muhimu ambazo zitakuongoza katika ufanyaji mazoezi yako. Istilahi nyingine utaendelea kujifunza kadiri ynavyoendelea kubobea katika mazoezi. REP : Hiki ni kifupisho cha neno Repeatition. katika mazoezi neno hili humaanisha kurudia kitendo flani. kwa mfano: mtu akisema 10 Reps, anamaanisha kufanya hicho kitendo husika mara 10. Kwa mtu ambae anapiga push up, akienda juu na chini amemaliza mara moja. hivyo 10 reps maana yake ni push ups 10. SET : H
Blog hii ni kwa ajili ya kukusaidia kutatua changamoto za ki afya ambazo zinaweza kutatulika kwa kubadilisha jinsi ya kula na mtindo wa maisha