Jinsi Ya Kukabiliana Na Kutibu Vidonda Vya Tumbo Vidonda vya tumbo hutokea pale ambapo sehemu ya kuta za kwenye umio (Oesophagus), tumbo au Utumbo kua na kidonda. Na hii hutokea baada ya kuharibika kwa Ute (mucus) ambao hulinda kuta hizo. Unaweza kusoma zaidi kuhusiana na Vidonda Vya Tumbo na dalili zake kwa kubofya HAPA Watu wengi hudhania ya kwamba bacteria anaefahamika kwa jina la H-pylori ni adui. Bacteria huyu sio adui yako, kwa sababu unaishi nae tangu siku unayozaliwa. Ila tu huleta shida pale ambapo tunakula lishe mbivu pamoja na mtindo mbaya wa maisha. Ni Kwa Nini Vidonda Vya Tumbo Hutokea? Matumizi ya pombe Matumizi ya Nafaka (wanga) zilizokobolewa Matumizi ya viungo vya kiwandani kama vile Royco Matumizi ya Mafuta ya Mbegu (vegetable oils) mfano mafuta ya alizeti Matumizi ya dawa za maumivu kama vile diclofenac na bufren Matumizi mabaya ya dawa za antibiotics Uvutaji wa sigara Kutokupata usingizi wa kutosha Kulakula hovyo au kila wakati (huvuruga uwiano wa uzalishwaji wa
Blog hii ni kwa ajili ya kukusaidia kutatua changamoto za ki afya ambazo zinaweza kutatulika kwa kubadilisha jinsi ya kula na mtindo wa maisha