Skip to main content

Posts

Showing posts from December, 2021

MAZOEA/TABIA 10 ZA KUJENGA UDHIBITI WA KUONDOKANA NA UNENE

  Ulaji na mtindo mbaya wa maisha husababisha unene. MAZOEA/TABIA 10 ZA KUJENGA UDHIBITI WA KUONDOKANA NA UNENE. Unene kupita kiasi ni tatizo la kiafya ulimwenguni kote. Uzito uliopitiliza ni kuwa na 10% hadi 19% zaidi ya uzito sahihi unaotakiwa kiafya. Wakati Unene kupita kiasi ni kuwa na zaidi ya 20% ya uzito sahihi unaotakiwa kadiri ya urefu, jinsia na ukubwa wa mifupa. Kiini cha tatizo hili ni kiasi kikubwa cha Kalori. Uzito huongezeka pale ambapo unakula kalori nyingi zaidi kuliko mwili wako uwezavyo kutumia. Kalori za ziada huhifadhiwa kama mafuta mwilini. Kwa kila kalori 3,500 za ziada inayopokelewa mwilini, nusu kilo ya uzito huongezeka. UZITO SAHIHI UNAOTAKIWA KUA NAO KULINGANA NA UREFU PAMOJA NA JINSIA. jedwali la uzito sahihi kulingana na urefu pamoja na jinsia. MAZOEA 10 YA KUJENGA UDHIBITI WA KUDUMU WA UZITO SAHIHI. Tumia vyakula vya mimea/nafaka ambazo hazijakobolewa, vyakula hivi hua na wingi wa nyuzinyuzi na viinilishe. (Ili kujua madhara ya nafaka zilizokobolewa, soma