Skip to main content

Posts

Showing posts from October, 2021

NJIA RAHISI JINSI YA KUANZA KUPUNGUZA UNENE/KITAMBI

  NJIA RAHISI JINSI YA KUANZA KUPUNGUZA UNENE/KITAMBI. Inakadiriwa ya kwamba, katika kila familia hapa Tanzania, hapakosekani walau mtu mmoja ambae ana uziro uliopitiliza. Yaani Obese. Wapo watu kadhaa ambao wamekua wakisema ya kwamba wao wana unene wa kurithi. Kwa sababu katika familia au ukoo wao wengi ni wanene. Lakini hili halina ukweli, Ila tu ni kwamba familia nyingi zinarithishana mtindo wa maisha. Na hivyo ndio maana unaweza kuona familia flani au ukoo flani wote ni wanene. Inapokuja swala la kupunguza unene, hamna njia za mkato kama ambavyo watu wengi hupendelea. Mtu anasahau ya kwamba hakunenepa ndani ya muda mfupi, bali alinenepa kwa muda mrefu. Lakini leo hii mtu atataka kupungua haraka sana ndani ya muda mfupi. ROMA HAIKUJENGWA KWA SIKU MOJA. Njia bora zaidi ya kupunguza Unene ni kwa kuzingatia ulaji sahihi pamoja na kubadilisha mtindo wa maisha kwa ujumla. Zipo dawa zinazosaidia kurahisisha safari ya kupunguza unene, lakini ieleweke ya kwamba, dawa hizi husaidia kurahisi