Erectile Dysfunction SABABU ZA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME Upungufu wa nguvu za kiume, ama kwa jina jingine Erectile Dysfunction (ED) ni ile hali ambayo mwanaume hushindwa kusimamisha uume au kushindwa kusimamisha uume kwa muda mrefu na kuweza kufanya tendo la ndoa. AU ni hali ya mwanaume kushindwa kusimamisha uume kabisa au kushindwa kusimamisha wakati wa kujamiiana hasa baada ya kufika kileleni. Na hali hii huweza kumtokea mtu yeyote. Kwa kawaida, kila mwanaume huweza kupatwa na hali hii walau mara moja katika maisha yake. Ingawa inapotokea mara kwa mara, basi hilo hua ni tatizo na linahitaji kutatuliwa. VISABABISHI VYA UPUNGUFU WA NGUVU ZA KIUME. Kisukari: husababisha kusinyaa kwa mishipa ya damu kwenye uume. Hivyo kushindwa kupitisha damu ya kutosha. Uvutaji wa Sigara: Nicotine iliyopo kwenye sigara husababisha kusinyaa kwa mishipa ya damu iliyopo kwenye uume. Hivyo kushindwa kuweza kusimamisha uume. Magonjwa ya moyo: husababisha mzunguko wa damu kwenye mishiba ya kwenye uume
Blog hii ni kwa ajili ya kukusaidia kutatua changamoto za ki afya ambazo zinaweza kutatulika kwa kubadilisha jinsi ya kula na mtindo wa maisha