Skip to main content

Posts

Showing posts from May, 2021

SAHANI YA MLO UNAOFAA

 SAHANI YA MLO UNAOFAA “Hati miliki © Chuo Kikuu cha Harvard. Kwa maelezo zaidi kuhusu Sahani ya Mlo Unaofaa, tafadhali tembelea Kitengo cha Lishe, Idaya ya Lishe, Chuo Kikuu cha Afya ya Jamii cha Harvard  http://www.thenutritionsource.org  na Majarida ya Afya ya Harvard, health.harvard.edu.” Sahani ya Mlo unaofaa , ambayo imebuniwa na wataalamu wa lishe kutoka Chuo Kikuu cha Afya ya Jamii, Harvard na kuhaririwa na wataalamu kutoka Harvard, ni muongozo wa mlo kamili unaofaa kwa afya-ikiwa utatumiwa kwenye sahani ya mlo ama kama chakula cha kufunga kwenye box. Bandika nakala kwenye fridge au kabati ili ikukumbushe kuandaa mlo kamili wenye afya! Sehemu kubwa ya mlo wako uwe mbogamboga na matunda – ½ ya sahani Hakikisha unaweka aina mbalimbali zenye rangi tofauti. Viazi mbatata havihesabiwi kama mbogamboga katika Sahani ya Mlo unaofaaa kwa sababu ya madhara yake kwenye kiwango cha sukari mwilini. Tumia vyakula vya nafaka isiyokobolewa – ¼ ya sahani Vyakula vinavyotokana na nafaka isiyokob